February 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Hollyland yafagiliwa ubora wa taaluma

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Chunya

SERIKALI mkoani Mbeya imesema kuwa miongoni mwa shule bora ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika taaluma ni pamoja na Shule ya mchepuo wa kiingereza ya Holly land iliyopo katika Mji mdogo Makongolosi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Kauli hiyo imetolewa Februari 10,2025 na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Juma Homera wakati alipotembelea shule hiyo kujionea maendeleo ya taaluma katika Shule akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya pamoja na chama cha Mapinduzi wilayani humo.

Lengo la kutembelea shule hiyo ni kuipongeza kwa matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji mkubwa wa Lawena Nsonda(Baba Mzazi).

Homera amesema kuwa miongoni mwa shule bora kabisa inayotoa elimu nzuri na kuwa walimu wanaofundisha kwa weledi mkubwa Shule ya Hollyland ni moja ya shule yenye taaluma ya juu kabisa kwa mkoa Mbeya .

“Hivyo nimpongeze sana ndugu yetu Lawena Nsonda (Baba mzazi)kwa kuwekeza hapa Makongolosi Sababu wazazi wengi wameleta watoto wao hapa kutokana na  ubora wa elimu unaotolewa katika shule hii hivyo nimpongeze sana mkurugenzi wa Shule hii kwa uwekezaji aliofanya  pia nipongeze juhudi kubwa za walimu katika ufundishaji wa watoto na endeleeni kufundisha vizuri zaidi ili wazazi walete watoto zaidi katika Shule hii”amesema mkuu huyo wa mkoa.

Akielezea zaidi Homera amesema kuwa serikali ya mkoa wa Mbeya inampongeza mkurugenzi wa Shule hiyo na itaendelea kuunga mkono jitihada zake za kutoa elimu bora  na ikitokea fursa yeyote ya kusapoti shule binafsi shule  basi Hollyland itakuwa miongoni mwa Shule ambazo zitafikiwa  huku akiutaka uongozi wa shule hiyo kuendelea kuwatunza vizuri watoto.

“Siku hizi kuna matukio ya utekaji wa watoto kama mliona mkoa fulani watoto wametekwa tunashukuru jeshi la polisi kwa kupambana na kuwaokoa watoto hivyo nawaomba msiruhusu watu wasiojulikana wanaoomba lifti kwenye gari za shule ambazo zinawarudisha watoto majumbani  uongozi wa shule waambieni madereva wenu kutoruhusu mtu yeyote kupanda gari za  shule “amesema Homera.

Kwa upande wake mkurugenzi  wa Holly landa  pre ande Primary school,Lawena Nsonda (Baba Mzazi) ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa kwa wawekezaji nchini wakiwemo wamiliki wa Shule.

Shule ya Holly Land ni moja ya shule bora ambayo imekuwa ikifanya vema  Kiwilaya,Kimkoa na Kitaifa katika taalum.