January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule 9 zapatiwa vyakula vyenye thamani ya sh.mil. 148.2.

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dk.Suleiman Serera, amepokea tani  78.2 za chakula pamoja na mafuta ya kula lita 2,220 kutoka World Vision  Tanzania kwa kuzipatia shule 9  za kata ya Ruvuremiti na Lobosoit wilayani humo vyakula vyenye thamani ya sh.mil. 148.2.

Akizungumza jana mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Ngage Andrea Daniel  Ndikoye, mratibu wa mradi wa Shirika la World Vision Tanzania Gloria Mashingia, wakati akikabidhiwa chakula hiko katika shule ya msingi Ngage Kata ya Loibosoit  chini ya diwani wake Siria Baraka Koduya, Mkuu hiyo aliishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa chakula uliolenga kuzisaidia shule 9 za Kata ya Ruvuma na Loibosoit.

Dk.Serera alisema Shirika laWorld Vision Tanzania limetoa chakula jumla ya tani zipatazo 78.2 cha chakula,  na kubainisha kuwa kati ya hizo tani 50.6 za mahindi na tani 27.6 za maharagwe huku mafuta ya kupikia lita 2,220 vyote vikiwa jumla ya thamani ya sh. Mil.148,2, msaada utakaotolewa kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu, a!hapo jumla ya wanafunzi wapatao 3696 watanufaika na msaada wa chakula.

Aidha amesema msaada huo umeletwa kufuatia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kuandika barua kwa Shirika hilo ikiomba kusaidiwa chakula cha wanafunzi mashuleni wa kata zilizoathilika zaidi na suala la ukame, kipindi ambacho wafugaji wengi wamepoteza mifugo yao.

” Kama mnavyofahamu wale wakulima, mnaweza kwenda shambani kulima mkiwa na njaa, wale wafugaji mnaweza kwenda kuchunga huku mkiwa njaa, au tujiulize mimi na wewe unawezaje kufanya shughuli yoyote ile ngumu tena inayohitahi kutumia zaidi akili  kufanya ukiwa na njaa si huwezi kufanya hivyo, tena hakuna kazi ngumu kama kusoma, hivyo watoto wanapokua wamepata chakula shuleni kutasaidia kuwajenga kiakili na hatimaye kuongeza bidii ya kusoma na kuinua kiwango cha ufaulu mashuleni” alisema Dk. Serera.

Aidha alifafanua kuwa akili na mbili ukichoka watoto hawataweza kusoma na kuelewa, watakua wa naomba tu muda wa vipindi uishe ili waweze kurudi majumbani kwao, huku wakiwa hakuna walichoingiza vichwani mwao, ambapo hata walimu nao watawezaje kufundisha watoto wakaelewa ili hali hawapati chakula.

” Jitihada iliyofanyika na World Vision Tanzania itawezesha sasa kuhakikisha kwamba changamoto hii inatatuliwa na sasa tunaweza kufika mbali zaidi, nitoe rai tu kwenu World Vision Tanzania msiishie hapa, kwani natambua kuwa mradi huu unaishia mwaka 2023, hivyo tuendelee kushirikiana na nikiangalia pale naona mna membo yenu katika darasa pale ” aliongeza Mkuu huyo wa wilaya.

Aidha aliwahakikishia Shirika hilo kuwa serikali inatambua michngo mikubwa inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo World Vision Tanzania , na hibyo itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika jitihada mbalimbali za kuhakikisha mambo yote yaliyopangwa yanaenda kama ilivyotarajiwa na sivingevyo.

” Nipo hapa sio kwasababu hii tu, lakini pia kuonyesha kwamba serikali yenu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ipo kazini na kazi inaendelea, inathamini kikamilifu jitihada na mchango mkumbwa unaotolewa na wadau mbalimbali ya maendeleo Kama ninyi World Vision,  hivyo nitakua mkali sana nitakapobaini chakula hiki kimetumika ndivyo sivyo , si mnafahamu kuwa chakula hiki kimeletwa kwaajili ya kutumika na wanafunzi na kusaidia kuchangia kukabiliana na upungufu wa chakula waliokua nao ” alisisitiza Dk.Serera

Kufuatia makabidhiano ya chakula hiko,aliwataka wanafunzi sasa kuhakikisha wanaongeza bidii katika masomo ili kuweza kuwatia moyo Wazazi, walezi walimu na hata wadau Kama hao wanaojitolea kuwasaidia chakula, kwani serikali   inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya kusoma, hivyo watakapofaulu wote mambo yatakua mazuri zaidi.

Akisoma taarifa fupi kwa Mkuu huyo wa Wilaya Mratibu wa Mradi huo Gloria Mashingia alisema Ofisi ya mkurugenzi wilaya ya Simanjiro iliandika barua kwa World Vision kupitia mradi wa Ruvu Remit kuomba kusaidiwa chakula cha wanafunzi mashuleni.

” Uongozi wetu wa shirika waliweza kuwatembelea viongozi wa wilaya ili kujadili hii changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo Moja ya changamoto zilizoelezwa ni wazazi kushindwa kuchangia chakula mashuleni kwa wakati kwasababu ya mifugo kufa iliyopelekea kipato cha kaya kupungua, hivyo World Vision kupitia Mradi wa Ruvu Remit iliona ni vyema ikatoa msaada wa chakula mashuleni hususani shule zilizopo tarafa ya Ruvu Remit ili kuhakikisha watoto wanapata chakula katika kipindi hiki ambacho wafugaji wengi wamepoteza mifugo yao, ” alisema Mashingia.

Aidha Mashingia alisema mradi huo umetoa msaada wa chakula mashuleni kwa miezi mitatu katika shule 9 (shule 7 za msing na shule 2 za sekondari) zilizopo tarafa ya Ruvu Remit, ambapo  kila mwezi mradi utatoa mahindi tani16.9, maharage tani 9.2 na mafuta ya kula lita 740 hivi vyote vina thamani ya Tsh 49,416,000.

“Msaada huu tutatoa kwa miezi mitatu ambayo ni mwezi wa tatu, mwezi wanne na mwezi wa tano, kwa miezi yote mitatu tutatoa kiasi cha tani 50.7 za mahindi, tani 27.6 za maharage na lita 2,220 za mafuta ya kula, Msaada huu wote kwa miezi mitatu una thamini ya Tsh 148,248,000. Jumla ya watoto 3696 watanufaika na msaada wa chakula” aliongeza Mratibu huyo.

Hata hivyo alisema Shirika la World Vision Tanzania linajihusisha pia na kusaidia kupambana na majanga mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo.

Mkuu wa wlaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dk Suleiman Serera akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Ngage Andrea Daniel  Ndikoye ( kushoto )  wakati wa makabidhiano ya chakula tani 78.6 za mahindi na maharage na mafuta ya kupikia lita 2,220 katika shule ya msingi Ngage Kata ya Loibosoit kilivhotolewa na Shirika la World Vision Tanzania, Mkuu hiyo aliishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa chakula uliolenga kuzisaidia shule 9 za Kata ya Ruvuma na Loibosoit, Picha na Mary Margwe
Mkuu wa wlaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Dk Suleiman Serera akizungumza jana mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Ngage Andrea Daniel  Ndikoye ( kushoto ) na wanafunzi wa shule ya msingi Ngage kata ya Loibodoit wakati wa makabidhiano ya chakula tani 78.6 za mahindi na maharage na mafuta ya