Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenye Ulamavu Tanzania(SHIVYAWATA) limeipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekuwa ikichukua dhidi ya kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Shirikisho hilo, Makamu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Tungi Mwanjala amesema kuna umuhimu wa kuendelea kuikumbusha Serikali mambo muhimu ambayo yapo kwenye miongozo na sheria kuhusu watu wenye ulemavu nchini.
Amesema kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ameviomba vyombo vya habari kuwa karibu na watu wenye ulemavu kwani kuna wawakilishi wao ambao wamepata nafasi na kwamba tangu mwaka 1995 hadi sasa mwaka 2020 kumekuwepo na ongezeko la watu wenye ulemavu Bungeni ni jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kundi hili nalo linakuwa na wawakilishi wa kutetea changamoto zao.
Mwanjala amesema nafasi zilizopo kwa kundi hilo ni tano ambapo Tanzania Bara wanazo nafasi tatu na Zanzibar nafasi mbili.
“Tulianza na mwakilishi mmoja lakini sasa wamefikia wawakilishi watatu kwa Tanzania Bara na watatu kwa Zanzibar na kweli ni kitu kizuri na tunaipongeza tunaipongeza Serikali yetu kwani imefanya jambo jema.Hata hivyo tunatamani tuwe na nafasi nyingi zaidi ya wawakilishi wa watu wenye ulemavu kwani shirikisho letu peke yale linavyama 10 na kila chama tunapenda kiwe na mwakilishi wake bungeni ili aseme yanayowahusu,”amesema.
Mwakilishi wa umoja wa Redio za Kijamii ,Saum Bakari amesema huu si wakati wa walemavu kujiona wanakuwa mstari wa mbele kwa kuamini wanaweza kwani kuna viongozi wengi wenye ulemavu wameonesha uwezo mkubwa katika utumishi na wamekuwa chachu ya maendeleo ya nchi yetu.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19