Na Jackline Martin, TimesMajira Online
SHIRiKA lisilo la kiserikali Maternal Care Foundation ( McF) limeendelea kufanya
jitihada za kuzuia vifo na ulemavu vinavyohusiana na ujauzito miongoni mwa wanawake na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Lengo la hatua hiyo ni kuboresha mazingira ya afya katika afya ya uzazi, na mtoto mchanga.
Akizungumza wakati wa maonesho ya afya ya wanawake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Maonesho
Mliman City, Afisa Mkuu wa Habari wa McF, Tesha Mbiligili, amesema wameendelea kusisitiza umuhimu wa uhamasishaji wa
jamii, elimu, na upatikanaji wa huduma za afya kwa ajili ya kufikia matokeo bora ya afya.
Lakini pia kuona haja ya kuwepo mbinu shirikishi kwa afya ya mama na mtoto.
“Katika hafla hii ilitolewa elimu ya afya bila malipo, huduma za upimaji na uchangiaji damu ili kushughulikia masuala muhimu
yanayoathiri afya ya mwanamke
na watoto chini Tanzania.”
“Hafla hii imeonesha nguvu ya ushirikiano na ari ya mashirika haya katika kuboresha maisha ya wanawake na watoto nchini
Tanzania.” alisema Tesha
Alisema kwa kuzingatia kukuza afya ya uzazi, afya ya akili, ukuaji wa watoto, afya ya uzazi na lishe, hafla hiyo imeleta pamoja mashirika mbalimbali ambapo kila
mmoja alichangia utaalimu wake ili
kuinufaisha jamii.
“Washirika wakuu katika maonesho hayo ni pamoja na, Shujaa Cancer Foundation,
N u r s i n g a n d M i d w i f e r y
Empowerment Organization, Mental Health Tanzania, Tanzania Epilepsy Organization, Watoto Afrika, Bright Jamii Initiative, Kaya
Foundation, Gorgeous Look Atelier, Hospitali ya CCBRT na Hospitali ya Sanitas.”
“Maonyesho ya Afya ya Wanawake
yalikuwa tukio la uzinduzi ambalo
linaonesha dhamira kuu ya McF ya
kuboresha matokeo ya afya kwa
wanawake na watoto. Hili lilikuwa juk waa la kuwawezesha wanawake na
watoto kwa taarifa sahihi za afya na rasilimali muhimu, na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya afya. Mpango huu unaondoa vikwazo vinavyozuia
upatikanaji wa taarifa muhimu za
afya ndani ya jamii,” alisema Tesha
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam