December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shilingi milioni 4.5 za fomu ya Rais zakusanywa Segerea

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli amefanya harambee ya fomu ya kumchangia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Kongamano la miaka mitatu ya Rais.

Harambee hiyo ya kumchangia Dkt.Samia ilifanyika katika Kongamano la Wanawake wa jimbo la segerea lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Bonah Ladslaus Kamoli.

“Wanawake wote wa Jimbo la segerea kura ya Rais tunampigia Dkt.Samia Suluhu Hassan na leo tumemchangia shilingi milioni 4.5 katika harambee yetu kwa ajili ya fomu ya Urais mwaka 2025 katika uchaguzi mkuu “alisema Bonah

Mbunge Bonnah amesema wanawake wa jimbo la segerea wote wameungana katika kuunga mkono juhudi za Rais na ifikapo mwaka 2025 wanampigia kura katika uchaguzi mkuu.

Alisema wanawake wa Segerea wapo kwa ajili ya kumpongeza Rais kwa kufanya mambo makubwa katika sekta ya Afya,sekta ya Elimu na Miundombinu ambapo kwa sasa jimbo la Segerea watoto wanasoma katika kata zao ambapo katika uongozi wake wa miaka mitatu ameboresha sekta ya Elimu na sekta ya afya wamejenga kituo cha afya KINYEREZI, Mnyamani, kata ambazo hazina kituo cha afya zahanati wanazipandisha hadhi pamoja na Hospitali.

Akizungumzia Changamoto za jimbo hilo alisema Miundombinu ya Barabara sio Rafiki awali kulikuwa na mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP mwaka 2010 na mwaka 2015 mradi huo ukapigiwa kura na madiwani wa upande wa pili mradi aujafika kwasasa Mradi unatarajia kurudi wa kujenga Barabara za kisasa ambapo unatarajia kuanza Aprili mwaka huu jimbo la segerea litakuwa la kisasa Barabara nzuri na Taa za Barabarani

Wakati huo huo alizungumzia mikopo ya Wanawake ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri alisema wanawake wengi wanategemea maendeleo lakini mikopo hiyo imewakatisha Tamaa Wanawake wa jimbo la segerea wamekosa mikopo wanapigwa danadana ambapo alitaka Danadana ziachwe wawezeshwe mikopo wampigie kura Rais.

Akizungumzia sekta ya Elimu alisema baadhi ya shule zinaendelea na michango ya wanafunzi shuleni hivyo ameomba Serikali kupiga marufuku.