January 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sheikh Zuber amjulia hali msama

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally,amemtakia afya njema Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandalizi pia wa Matamasha Makubwa ya Pasaka Alex Msama baada ya kuugua ghafla ambapo amemtakia afya njema na kupona haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kulijenga Taifa la Tanzania.

Sambamba na kumtakia kheri Mkurugenzi Alex Msama Mufti Mkuu huyo amesema kwamba jamii inatambua mchango wake mkubwa kwa kwa kuisaidia jamii kupitia matamasha yake ambayo amekuwa akiyaanda kazi ambayo pia huambatana na mchango wake kwa taifa katika kuleta maendeleo.

Aidha Sheikh Mkuu ametumia pia siku ya leo ya Eid jamii kuungana na wagonjwa mbalimbali kwa kuwaombea wapone haraka kwa ajili ya kurejea katika afya zawo ili warudi katika kazi zawo waendelee kulijenga taifa lao.