Na Penina Malundo,Timesmajira
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania ,Sheikh Ponda Issa Ponda kujiunga rasmi na Chama cha Act Wazalendo leo ambapo ni mara ya kwanza kwake kujiunga na Chama cha siasa nchini Tanzania .
Mamia ya wanachama wa Chama hicho pamoja na watanzania mbalimbali wameweza kuhudhuria mapokezi ya Sheikh Ponda katika Ofisi za Chama hicho Makao Makuu Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Mapokezi hayo ya Sheikh Ponda yameongozwa na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama hicho pamoja na Ngome zake .

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema wamefurahia sana na ujio wa Sheikh Ponda katika chama chao kwani kila jambo linawakati wake.

Amesema Sheikh Ponda anafahamika kwa mengi katika uwanja wa siasa na jina lake sio ngeni kwani kuna nyakati alipanda katika majukuwaa mbalimbali ya kisiasa ikiwemo Chama cha Wamanchi CUF pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.


More Stories
Kiongozi wa Mwenge apongeza wananchi kupelekewa huduma ya maji Handeni
TFS yawakaribisha wawekezaji katika vivutio vya utalii wa misitu
Waziri Bashungwa:Tumieni teknolojia za kisasa kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka