January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shamsa Ford ashusha ujumbe mzito

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MUIGIZAJI wa filamu na Mjasiriamali hapa nchini Shamsa Ford, ametoa ujumbe mzito kwa jamii na kuwataka kuombeana mema pindi binadamu mwenzao anapopata matatizo ya kudunia.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Shamsa amesema, kuna kipindi mwanadamu huwa anapitia changamoto mbalimbali hivyo ni vyema kumpa moyo pindi anapotwa na mitihani.

“Huwezi kuelewa maumivu ya mwenzio mpaka yakukute. Tuishi kwa kuoneana huruma na kuombeana mema jamani, mwenzako anapopitia mitihani tusiwe wa kuhukumu hata wewe unaweza ukapitia, kama bado unaishi duniani ni kumuomba tu Mungu atuepushe na mabalaa hakuna anayeijua kesho yake,” ameandika Shamsa.