Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amewataka viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kuacha ukimya badala yake watoke kueleza mafanikio ya serikali.
Shaka alisema hayo leo mjini Babati katika mkutano wa ndani wa kujitambulisha mbele ya wanachama wa CCM, akiwa mlezi mpya wa Chama katika Mkoa huo, akichukua nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
“Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya kote nchini mna jukumu la kuyaeleza mafaniko ya serikali ya mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan), sasa hivi kuko kimya hamumtendei haki Rais wetu,” alisema.
More Stories
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana