October 28, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SGA Cash in Transit yatajwa kuwa kampuni bora ya huduma

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

SGA Cash in Transit Tanzania imetajwa kuwa Kampuni Bora ya Huduma za Courier na Uwasilishaji wa Mwaka katika Tuzo za Supply Chain, Mobility & Logistics (SML) 2026.

Tuzo hiyo inatambua ubora, uaminifu na kiwango cha huduma katika sekta ya courier, na inaonyesha dhamira ya SGA ya kusafirisha fedha na vitu vya thamani kwa usalama, ulinzi na kwa wakati kwa wateja kote nchini Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security Tanzania, CPA Jonathan Geleta, amesema ushindi huo ni uthibitisho na pia changamoto. “Utambuzi huu unaonyesha viwango ambavyo tumejenga biashara yetu juu yake, lakini pia unainua kiwango cha matarajio. Wateja wetu wanatarajia zaidi kutoka kwetu kila mwaka, na tutaendelea kuboresha huduma zetu na kuwekeza katika watu wetu, michakato na teknolojia ili kukidhi matarajio hayo nchini kote Tanzania,” amesema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Huduma za Courier,Stella Chiwango, amesema utambuzi huo unaonyesha kujitolea kwa timu zinazohusika na kuhakikisha huduma za courier zinazotegemewa.

“Huduma za courier ni kutimiza ahadi: kumfikishia mtu sahihi mzigo sahihi kwa wakati sahihi. Tuzo hii inatambua nidhamu na kujitolea kwa wasafirishaji wetu na timu za usambazaji, na inatutia moyo kuendelea kuboresha huduma tunazowapa wateja wetu,” amesema.

Mkuu wa Huduma za Cash in Transit, Bw. Rashid Kawawa, amesema utambuzi huo unasisitiza umuhimu wa nidhamu ya kiutendaji na usalama katika kutoa huduma salama za usafirishaji.

“Nyuma ya kila uwasilishaji salama kuna timu inayopanga kwa umakini, inayofuata taratibu zilizowekwa na isiyowahi kuhatarisha usalama. Najivunia watu wetu na ninawashukuru wateja wetu kwa imani wanayotuwekea,” amesema.

Tuzo za SML ni jukwaa la hadhi ya juu katika sekta, linaloadhimisha utendaji bora, ubunifu na matokeo chanya katika sekta za ugavi (supply chain), usafiri (mobility) na usafirishaji (logistics). Toleo la mwaka huu liliwakutanisha kampuni za usafirishaji, waendeshaji wa minyororo ya ugavi, wabunifu katika sekta ya usafiri, mitandao ya usambazaji, taasisi za fedha, kampuni za bima na watoa huduma.

Tuzo hii inaimarisha dhamira ya SGA ya kudumisha viwango vya juu vya usalama, uaminifu na utoaji wa huduma katika shughuli zake za courier na usafirishaji wa fedha (cash in transit).

SGA Cash in Transit (T) Limited ni kampuni iliyosajiliwa mwaka 1995 kama Group Four Cash in Transit (T) Ltd, ikawa Security Group Cash in Transit (T) Ltd mwaka 2000, kisha ikabadilisha chapa na kuwa SGA Cash in Transit (T) Ltd mwaka 2016. Kwa miongo mitatu, imejijengea sifa katika usafirishaji na utunzaji salama wa fedha na vitu vya thamani kwa taasisi kuu za fedha, ikiungwa mkono na rasilimali na uzoefu iniwa mojawapo miongoni mwa makampuni ya SGA.

SGA imethibitishwa kwa viwango vya ISO 9001:2015, ISO 45001:2018, ISO 14001:2015 na ISO 18788:2015, na ni mwanachama wa International Code of Conduct Association (ICoCA).