Judith Ferdinand na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Christopher Ngubiaga,amesema ni wajibu wa Serikali na wadau wa maendeleo,kuhakikisha wanazingatia haki za vyombo vya habari na waandishi wa habari,ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira salama kwa uhuru pamoja na kupewe taarifa za maendeleo wanazozihitaji kwa wakati.
Ngubiagai,amesema hayo Desemba 13,2024kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mtanda,katika hafla ya ,usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari Mkoa wa Mwanza, iliofanyika jijini hapa,ambayo ilibeba kauli mbiu isemayo,”Maendeleo ya pamoja kupitia uhuru wa vyombo vya habari,”.hafla hii ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka wa MPC, ambao unalenga kuimarisha uhusiano kati ya waandishi wa habari na wadau.
Pia amesema,waandishi wa habari wanalo jukumu la kudhibiti na kufuatilia miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha na rasilimali za umma zinatumika kwa manufaa ya wananchi.
“Mkoa wa Mwanza,una fursa nyingi za kuboresha huduma za afya,elimu na miundombinu,hivyo vyombo vya habari vina jukumu la kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki mchakato wa maendeleo,kudhibiti matumizi na kufuatilia miradi ya maendeleo kuhakikisha fedha na rasilimali za umma zinawanufaisha wananchi,”.
Pia ameeleza kuwa,Serikali inatambua changamoto za vyombo vya habari,ikiwa ni pamoja na ukosefu wa rasilimali,usalama wa waandishi wa habari, huku vinakumbana na shinikizo kutoka kwa wadau mbalimbali.Hivuo ni muhimu zikatatuliwa kwa ushirikiano wa Serikali,vyombo vya habari na wadau wengine katika jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC),Edwin Soko,amesema nguvu ya vyombo vya habari inafahamika,hivyo vitaendelea kufanya kazi kwa uzalendo kwa maslahi ya wananchi na kuomba wapewe taarifa za maendeleo kwa wakati bhadala ya kuzizuia.
Aidha,katika hafla hiyo wadau wa habari ambao ni TASHICO,NHIF,TCRA, PSSSF,NSSF,TIRA na PCCB walitumia fursa hiyo kueleza shughuli zao kabla ya kutunukia vyeti vya shukurani kutokana na michango yao kwa tasnia ya habari.
More Stories
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa