Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Mbeya
Imeelezwa kuwa ujio wa ndege kubwa ya mizigo katika Mkoa wa Mbeya itachochea pato la Taifa ,ajira kwa vijana pamoja na uhakika wa masoko ya mazao ya wakulima mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Beno Malisa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Juma Homera wakati wa Kikao cha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kukutana na wadau wa Usafiri kuwaeleza ujio wa ndege kubwa ya mizigo aina ya boing 767-300 F yenye uwezo wa kubeba tani 54 kwa wakati mmoja.
Mallisa amesema kuwa ujio wa ndege hiyo unaifanya Tanzania kuingiakwenye historia ya biashara ya ndege ya mizigo ambayo sio tu kwaAfrika Mashariki bali kwa ngazi ya kimataifa.
‘’Lakini ndugu zangu mkoa wa Mbeya tunaangalia ndege hii kwa mtazamompana zaidi biashara ya mizigo ni ukweli usiopingika kuwa manufaaya ndege hii yatainufaisha wakazi wa mbeya na wananchi wa Tanzaniakwa ujumla ‘’amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha Mallisa amesema kuwa mahitaji ya soko duniani kwa mujibu waRipoti ya soko la usafilishaji wa mizigo ya 2023 ukubwa wa soko lamizigo umekua kutoka $191.01 bilioni mwaka 2022 kufikia $199.09 bilioni kwa mwaka 2023 kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka (CAGR) sawa na asilimia 4.2 .
Amesema uwepo wa ndege hiyo unaongeza ukuaji wa soko la usambazaji wa mizigo kufikia $224.78 bilioni mwaka 2027 kwa kiwango chaCAGR 3.1.
‘’Tumieni mkutano huu kama kioo cha kujithamini maandalizi yenu yaujio wa ndege ndege mpya ya kwanza ya mizigo kupitia mrejeshoutakaotolewa na wadau wenu ,pia mapungufu ambayo mtaambiwa na wadauwenu katika majadiliano hakikisheni mnayafanyia kazikikamilifu’’amesema Mkuu wa wilaya ya Mbeya , Beno Mallisa.
Cassim Mambo ni Mkaguzi mkuu wa ndani wa kampuni amesema kuwaserikali inashambulia kila sehemu ili kuhakikisha uchumi wa wananchiwake unakua kwa kasi na hilo linawezekana na kwamba bila bila miundombunu uchumi hauwezi kusogea .
‘’Serikali inatekeleza wajibu wake kwa kufanya uwezeshaji ili uchumi wa watu mbali mbali uweze kupita bila miundo mbinu uchumi hauwezi kusogea ndio maana tulisema usafirishaji ni nyezo mojawapo ya uchumi kuweza kukua kwa uchumi na fursa naamini kuwa ndege hii kubwa ya tani 54 kituo kimojawapo cha Mbeya kinaweza kuzalisha mizigo mingi zaidi’’amesema
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Ndege Tanzania(ATCL)Patrick Ndekana amesema kuwa lengo la kuja Mbeya ni kuona jinsi gani wanaweza kuboresha huduma za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga kwenda nchi jirani.
Mambo amesema kuwa ndege hiyo ya mizigo ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja ina masafa makubwa ambayo ni umbali wa kilometa 11,600.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano