March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yazindua nembo ya made in Tanzania

Na Irene Clemence,Timesmajira

SERIKALI imezindua nembo kitaifa ya made in Tanzania na kusisitiza kuwa ni alama ya utambulisho wa bidhaa na huduma ambazo zimekuwa zikizalishwa nchini kwa matumizi ya soko la ndani na la Kimataifa.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Julai, 8,2025 katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam, Naibu Waziri wa Viwanda n Biashara, Exaud Kigahe amesema uzinduzi wa nembo hiyo umefungua ukurasa mpya katika masoko ya kimataifa.

Amesema kupitia nembo hiyo bidhaa zitakuwa na utambulisho mmoja unahoakisi fahari ubora na hadhi ya bidhaa huku wafanyabiashara wakinufaika pamoja kuongeza thamani ya bidhaa na kuitagaza Tanzania kwa sura chaya kimataifa.

“Nembo ya made in Tanzania ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya Serikali na sekta binafsi na wadau wa Maendeleo na watanzania kwa ujumla”amesema Kigahe

Kigahe amesema nembo hiyo itakuwa ikitumika kwa njia ya kidigitali hivyo amesema ni muhimu kuendelea kuamasisha watanzania kujisajili kupitia mfumo unaoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade).

Aidha aliwataka wazalishaji wote wa bidhaa nchini kuipokea nembo hiyo kwa mikono miwili na kuipa nafasi katika kila bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Pia amewaomba wazalishaji wa bidhaa na watoa huduma kuhakikisha wamekilisha taratibu walizopewa na Tantrade na kuweka nembo katika bidhaa zao ili ziwekuwa na alama ya ulinzi.

“Bidhaa nyingi zaidi ya asilimia 60 zinatoka Tanzania hivyo ni muhimu kujitagaza ili watu waweze kujua …tutahakikisha watu wanatumia nembo hii iweze kuwa sehemu ya ubora na ulinzi “amesema

Katika hatua nyingine Kigahe aliitaka Tantrade kuhakikisha inaendelea kutumia teknolojia za kisasa kwa kuhakikisha bidhaa zinasajiliwa na kuonekana katika kanzi data ya kimataifa ili walaji wote waweze kuzitambua na kuziamini.

“Matarajio ya Serikali ni sekta binafsi, makampuni ya ndani kuendelea kuunga mkono juhudi hizi na kuchochea matumizi ya nembo katika bidhaa zote zitakazowasilishwa nchini”amesema Kigahe

Adha amewaomba wafanyabiashara kutumia nembo hiyo ipasavyo kwa ajili ya Maendeleo endelevu ya Biashara na uchumi wa Nchi.