November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yawataka wazazi kuiacha Mahakama kumaliza kesi za kijinai

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka Wazazi na walezi Jijijini Tanga kuacha tabia ya kumaliza kesi za kijinai nyumbani kwa ngazi za kifamilia na kaya kwa kuwa hawana mamlaka ya kumaliza kesi hizo na badala yake wametakiwa kuiachia mahakama kufanya kazi yake.

Hatua hii imekuja mara baada ya wazazi na walezi jijini Tanga kuwa na tabia ya kumalizana kinyumbani jambo ambalo linalowakosesha haki watendewa wa makosa hayo.

Mgumba ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria jijini Tanga ambapo amesema wao kama serikali wataendelea kuchukua hatua stahiki kwa wahalifu wote wanaoendeleza kufanya vitendo vya kihalifu kwa watoto wao na hata watoto wa kike.

Mgumba amelaani vikali vitendo hivyo na kusema serikali Mkoani Tanga inaendelea kuchukua hatua stahiki kwa wahalifu wote wanaoendeleza vitendo vya ukatili kwa watoto na jamiii kwani ukatili Tanga haukubaliki na serikali Mkoani Tanga imejipanga kukabiliana na vitendo hivyo hususani kwa wananchi wote wanaokikuka sheria.

“Kwanza nalaani Kitendo hiki cha wazazi kumalizana wenyewe kwa wenyewe ni kosa kisheria kwanza hawana mamlaka nalo na si jukumu lao ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu na ni kosa la kijinai na kinyume na katiba yetu suala hili ni jinai kama jinai zingine makosa yote ya kijinai mshatikiwa na malalamikaji ni jamuhuri ya muungano wa Tanzania wazazi, muathirikaa wao ni mashahidi tu.”

Aliongeza kuwa “Sasa wazazi muathirika wao watakuwa tu ni mashahidi kutoa ushahidi wao kwahiyo mlalamikaji ni serikali kwa msingi huo wazazi hawana mamlaka wala sheria ya kumaliza, jambo hilo wenyewe kwa wenyewe na hata ikitokea baba mtu ndio kafanya jambo hilo kwa mtoto wake bado ni mkosaji na ni muhalifu kama wahalifu wengine hivyo nitoe rai kwa wananchi kuacha tabia ya kumalizana wenyewe kwa wenyewe”alisisitiza Mgumba.

Mgumba amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha ndoto za watoto wao zinatimia hivyo kupitia wiki hiyo ya sheria wazazi waende wametakiwa kwenda kupata elimu katika mambo ya kisheria ilo kusaidia jamii.

“Sisi kama serikali tutaendelea kuchukua hatua kwa wahaligu wote wanaofanya vitendo vya kikatili kwa jamii ya wanatanga moja ya mikakati waliyonayo ni kuboresha mazingira ya jamii ya wanatanga ili kuwanusuru na vitendo hivyo.”

Aidha Mgumba amesema kuwa uwepo wa migogoro iliyokithiri hakuna ustaei wa jamii wala amani na hivyo ilikuimarisha uchumi imara ni vyema kuepuka migogoro isiyokuwa na tija na ulazima ilikuvutia wawejezaji nchini.

“Kama mwekezaji hana uhakika na uwekezaji wake kuja kuweja sehemu ambayo anaamini hakihaitemdeki sawasawa hakuna mwekezaji anaweza kuja kuwekeza Tanga na Taifa letu kwasababu atakuwa na hofu ya kuwekeza kama mfumo wa utoaji haki tuliokuwa nao ambao unaaminika ndani na nje ya nchi ndio unaovutia wawekezaji kuje kuwekeza, katika nchi yetu kwajiliya kutoa ajira, kujenga kipati kwa wananchi wetu, “alisema Mgumba.

Kwa upande wake Naibu Msajili wa mahakama kuu kanda ya Tanga mheshimiwa Beda Nyaki alisema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza ili waweze kupata elimu ya Sheria itakayowawezesha kujua haki zao za msingi 𝗂𝗅𝗂 𝗄𝗎𝗌𝖺𝗂𝖽𝗂𝖺 kupunguza malalamiko katika jamii.

”Mahakama inaadhimisha siku hii kwa niaba ya wananchi wote,tunatoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu haki zao,ili kujua haki zao ni lazima wawe na elimu na ufahamu,vinginevyo ndio unakuta wengi wanadhulumiwa”alisema Nyaki.

Aidha Nyaki ameeleza kuwa watu wengi wanahofu kuhusu kujua Sheria,lakini ni vema kujua Sheria na taratibu za Mahakama kwa kuwa utakapojua haki yako ni ngumu kupotea.

”Watu wengi hawana mwako wa kutafuta elimu ya Sheria wanakuwa na hofu,tunataka watu waamke popote ulipo,jifunze Sheria,jifunze taratibu za Mahakama,ili kupunguza migogoro ambayo inaweza kutatulika”alisema Nyaki.

Pia ameeleza kuwa,Mkoa wa Tanga umekua na migogoro mikubwa kwenye ardhi na mirathi watu wengi wamekuwa wakidhulumiwa kwa kuwa wamekuwa hawajui taratibu zinazotakiwa kufuatwa.

“Watu wengi sana wamekuwa wakidhulumiwa kwenye mirathi,hatuna muda mrefu wa kufundisha lakini wiki hii moja wakijitokeza wanaweza kupata mwako wa kujua sheria na badae akaendelea kutafuta elimu”alisema Nyaki.