Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SERIKALI imewataka wananchi hasa Wafanyabiashara Wenye maeneo ambayo hayana hati miliki kusajili maeneo yao ili waweze kupata hati hızo ambazo zitawawezesha kuzitumia kuomba mikopo kwenye sekta za kibenki na taasisi za kifedha ili waweze kuendeleza biashara zao.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu Wa Wilaya ya Tameke Mubale Matinyi wakati wa uzinduzi wa Clinic ya ardhi kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki ardhi uliopo chini ya world bank ulioenda sambamba na zoezi la utoaji hati ambapo alisema hata miradı yote inayotekelezwa na Serikali nchini ikiwemo ya umeme, mafuta na gesi lazıma iwe na hati miliki ya ardhi Kwani bila hati hiyo haiwezi kutekelezwa.
“Serikali ndiye mmiliki mkubwa wa ardhi, pamoja na umiliki huo Bado inatafuta hati, hivyo Kila mfanyabiashara ni vyema akawa na hati miliki”
Aidha amesema kukosekana Kwa Mfumo na utaratubu mzuri wa kumilikisha ardhi hapo awali kulisababisha kero Kwa wananchi hivyo uwepo wa mifumo ya kısasa ya kidigitali umeiwezesha Serikali kupitia Wizara ya ardhi kuwafikia wananchi Hadi Kwenye maeneo Yao na kuwapa hati miliki za ardhi.
“Suala la umiliki wa ardhi nchini ni ukosefu wa mfumo na utaratibu mzuri wa kurasimisha umiliki, kukosekana huko kunakuwa na kadhia nyingi kwa wananchi mojawapo ikitokea kuna suala la mirathi watu wanaanza kuvutana”
Kwa Upande wake kamisha wa ardhi mkoa wa Dar es Salaam Rehema Mwinuka amesema Serikali inania ya dhati ya kutatua kero za ardhi Kwa wananchi Kwa kuja na miradi mbalimbali ikiwemo wa uboreshaji usalama wa milki Ardhi.
Aidha amewaomba wananchi Wenye mashauri mbalimbali ya ardhi mahakamani kuyatoa mashauri Hayo na kuyawasilisha kwenye mradi huo ili yaweze kushughulikiwa na kupata hati zao.
“Wananchi ambao Wana migogoro midogomidogo ambayo wameipeleka Mahakamani na semehu zingine kufika ili yaweze kushughulikiwa kwani mradi huo una hatua mbalimbali ikiwemo utoaji elimu, utoaji wa Hati kwa vipande vilivyokamilika n.k”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Veronica Malangwa ameeleza kwamba zoezi la utoaji hati litapita katika mitaa mitano ya halmashauri ya Temeke na watatoa hati 3244 hivyo kusaidia kupunguza keto za wananchi na kuboresha milki zao.
“Tumepata ufadhili wa Benki ya Dunia ili kuweza kumaliza suala la urasimishaji ardhi ambalo kwa kiasi Fulani limekua ni kero kwa wananchi
Zoezi hili la utoaji hati limeanza hapa mbagala kuu Mashariki lakini kuna mitaa mitano itapitiwa na zoezi hili la utoaji hati ikiwemo kisewe, mwembe bamia, buza na mianzini”
“Tunategemea katika mitaa hii mitano tutatoa hati 3244, kwa kiwango hicho tutakua tumepunguza zaidi kero za wananchi na kuboresha miliki zao na hivyo kuwa na usalama wa kutosha na wataweza kujiinua kiuchumi”
Naye mwakilishi kutoka world bank amabao ndiyo wafadhili wa mradi huo Aisha Masanja ameipongeza Serikali Kwa kuwezesha kupatikana Kwa miradi hiyo ambayo ni chachu ya Maendeleo ya taifa na kwamba mradi umefadhiliwa Kwa jumla ya shilingi bilioni 345 na utafanyika katika halmashauri zote za mkoa wa dar es salaam.
“Mradi huu unafadhiliwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 345 na hizi zinafanya mradi huu katika Halmashauri 41 ndani ya nchi nzima ambapo kwa sasa zimeingezeka Manispaa 15 ndani ya Dar es Salaam
Mradi huu lengo lake ni kuhakikisha kwamba changamoto zote za urasimishaji zinafika mwisho”
Aidha amesema wana hatua mbalimbali ambazo wanaenda kuzitekeleza katika mradi huo, ikiwemo kutambua vipande vya ardhi vilivyotambuliwa, vipande vya ardhi ambavyo havijapimwa, wananchi ambao maeneo hayo muingiliano wa ramani, zote zitafanyiwa kazi na hatimaye kuhakikisha vipande vya ardhi laki sita vilivyotambuliwa vinaenda kumilikishwa.
“Mradi huu pamoja na kupanga na kupima vipande vya ardhi, una malengo mengine ya kuboresha miundombinu ya Sekta ya ardhi kwa nchi nzima ikiwemo majengo ya ofisi za ardhi katika mikoa 25 ndani ya nchi nzima.”
Amesema kwa sasa wanahama kwenye ardhi ya majalada na wanakwenda kwenye ardhi kidigitali ambapo watahakikisha Kila Halmashauri inafungiwa mifumo hii kwaajili ya utoaji wa Hati hizo kuhakikisha milki zinakua salama.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi