Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Dkt .Julieth Banigwa, amezindua kampeni ya Utunzaji Mazingira kwa kupanda Miti Segerea Wilayani Ilala .
Diwani Baningwa amezindua Kampeni hiyo katika kuunga Mkono Juhudi za Serikali katika suala zima la utunzaji Mazingira ambapo amezindua kampeni hiyo iliyopewa jina la Segerea ya kijani kwa kushirikisha Wanafunzi na klabu zao za Mazingira za sekondari ya Migombani ,Ugombolwa na Viongozi wa chama Jumuiya na Serikali .
“Suala la utunzaji Mazingira ni jukumu letu sote nimezindua Kampeni hii ya Segerea ya Kijani Ili kuunga Mkono Juhudi za Serikali katika suala la Mazingira na kutunza vyanzo vya maji “alisema Banigwa .
Diwani Banigwa alisema kampeni hiyo ya upandaji miti Segerea ambayo amezindua itakuwa endelevu kupanda miti katika wilaya ya Ilala .
Amewataka Wananchi na Wanafunzi wa shule hizo kuwa mabalozi wazuri wa kutunza miti hiyo ili kufikia malengo ya serikali .
Aidha aliagiza kila kaya kupanda miti ya matunda na vivuli katika maeneo yao Ili kuunga mkono Juhudi za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi Ili nchi.
Alitumia nafasi hiyo pia Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani katika miradi ya Maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu ,Barabara ,Miundombinu na Sekta ya Afya Rais Samia amefanya mambo makubwa amewataka viongozi wa chama na Jumuiya kutangaza kazi zinazofanywa na Serikali.
Mkuu wa Shule ya Ugombolwa Halima Nungu alimpongeza Diwani Julieth Banigwa kampeni yake ya mazingira ambayo amezindua Segerea na kushirikisha pia Wanafunzi waweze kujua umuhimu wa mazingira .
Mwalimu Halima Nungu alisema shule hiyo ina wanafunzi 919 Walimu 31 changamoto iliyopo madarasa machache idadi ya Wanafunzi kubwa ameishauri serikali ibadilishe majengo hayo kuwa golofa Ili waweze kujenga madarasa ya kutosha .
Aidha akizungumzia kitaaluma alisema Kila mwaka shule hiyo inafanya Vizuri .
Katibu wa chama Cha Mapinduzi Migombani Mfaume Said alisema anaipongeza Serikali na Diwani Banigwa Segerea kuzindua kampeni ya upandaji miti na kutoa elimu ya mazingira kwa kushirikisha klabu za Wanafunzi shule katika shule hizo.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango