November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yatoa mwongozo Kwa walimu wakuu wa Shule juu ya mvua zinazoendelea kunyesha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

KUFUATIA Mvua zinazoendelea kunyesha Serikali imetoa mwongozo kwa walimu wakuu kuchukua hatua za haraka na kutoa maamuzi wakati wanapoona hali mbaya ya hali ya hewa kwa kuwaruhusu watoto mapema.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa katika baadhi ya maeneo nchini.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam Aprili 24 ,2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kutokana na hewa ya hewa inayoendelea ni muhimu kuchukua hatua zaidi kutokana na miundombinu kuaribika.

“Nawaomba walimu na mnapoona hali ya hewa imebadilika kuchukua hatua za haraka kwa kuwaeuhuru watoto mapema kwenda nyumbani “amesema Profesa Mkenda

Pia amewaomba wazazi na walezi kuwakataza watoto kwenda shule pindi wanapoona hali ya hewa sio nzuri.

“Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ni vyema wazazi wakachukua taadhari ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza “amesema

Aidha ametoa onyo kwa madereva wa magari ya shule kutopitisha magari hayo kwenye mabwawa ya maji au sehemu yenye maji mengi ili kuepuka kuhatarisha maisha ya wanafunzi.

Pia amesema serikali kupitia wizara inawasilina na Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) hewa kuona kama kuna umuhimu wa kuweza kuchukua hatua zaidi .

Vilevile Profesa Mkenda amezipongeza shule binafsi ambazo zimeamua kusitisha masomo kutoka na hali ya hewa mbaya.