Na Bakari Lulela,Timesmajira
WAJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha Mapindizi (CCM) wamepatiwa mafunzo maalumu yenye lengo la kukizungumzia vema chama chao na harakati zao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akifungua mafunzo hayo Diwani wa chama cha Mapindizi (CCM) Saad Kimji amesema kuwa wajumbe ndio kioo cha chama hivyo yaeleweni vizuri hayo ili mkakizungumzie vizuri chama cha CCM.
“Mafunzo haya myasikilize vizuri ili kuweza kuyabeba yote yatakayo zungumziwa hapo muweze kuyafikisha kwa wananchi ambao ni wapiga kura,” amesema Kimji
Aidha kutokana na umuhimu wake katika kazi zenu za chama ningependa muwe watulivu Ili muweze kuyachukua Yale yote yaliyokuwa katika ilani ya chama cha Mapindizi (CCM).
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Katibu wa siasa na ujenzi wa wilaya ya Ilala Mwinyimkuu Sangaraza amesema kuwa maudhui ya mafunzo hayo ni kuwandaa viongozi ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hata hivyo elimu kwa wajumbe ina jukumu la kuwaongozea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao, kubwa zaidi ni kumsemea vizuri Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kazi azifanyazo.
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM