Na Hadija Bagasha Tanga,
Serikali imeelekeza watendaji wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kutafuta namna ya kuongeza muda wa matazamio ya miradi yao kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kwa sasa ili kuweza kuwabana makandarasi wanaojenga chini ya kiwango kinachotakiwa.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhandisi Geofrey Kaseskenya wakati wa mkutano wa 16 wa baraza la wafanyakazi wa Tanroads lililofanyika jijini Tanga na kushirikisha watendaji wa Tanroads nchi nzima.
Naibu waziri huyo amesema miradi yote ya barabara inayojengwa inakosa uwiano wa usawa na fedha iliyotumika hivyo ni vyema wakaangalia uwezekano wa kuwa na muda mrefu kwa wakandarasi hao kwani barabara nyingi zimekuwa zikifeli kutokana na muda mdogo ambao wamekuwa wakipewa wakandarasi kusimamiaambapo amependekeza wapewe barabara hizo wanazozijenga kuzisimamia ndani ya miaka 15.
“Ndani ya mwaka mmoja mtu anaweza kufanya chochote barabara isifeli lakini baada ya hapo mwaka wa pili barabara imeharibika ndio maana serikali imeona ipo haja ya kuja na mpango huo ili waweze kujenga kwa kiwango na ubora kulingana na fedha wanazopatiwa, “alibainisha Naibu waziri huyo.
Aidha Naibu waziri Kasekenya amewataka watendaji hao wa Tanroads kuendelea kutumia miongozo iliyopo katika kuzuia na kudhibiti rushwa katika manunuzi ya umma na rushwa kwenye mizani kwani kazi zao zinahusisha miradi mikubwa hivyo wajiepushe na mambo ya rushwa.
Tuna sheria ya manunuzi ya mwaka 2021 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2016 ambayo ni sura ya 16 na 83 watu ambao wanajenga barabara chini ya kiwango sheria inawataka wawe blacklisted waondolewe na wasipewe miradi yetu tena lakini pia sheria namba 83 inasema kama kuna watu wanaojihusisha na rushwa ama kampuni inayofanya miradi yetu inajihusisha na rushwa hao pia wanatakiwa waondolewe na wasifanye kazi tena wala kusimamia kazi kama hiyo na hata watendaji wanaomsimamia pia wawajibishwe, “amesisitiza Mhandisi Kasekenya.
Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza watendaji wa Tanroads kwa namna wanavyoshirikiana katika utendaji wao na kuweka usawa katika majukumu yao hususani katika mikoa yote Nchini.
Kwa upande Mtendaji Mkuu wa Tanroads… .amekiri kuwa kweli wameona tatizo la barabara zikikamilika, zimekuwa zikiharibika mapema na kusema ni tatizo la muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Amesema baada ya kuona tatizo hilo la ubora ikawalazimu waanze kufanya tafiti ya kwamba kwanini barabara zinaharibika mapema hivyo wakatumia kampuni kutoka nchini South Afrika kwajili ya kufanya utafiti wakabaini kuna baadhi ya maeneo mengine ni sababu ya lami wanayotumia.
Awali mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameomba serikali kujenga barabara ya kutoka Handeni-kibirashi kwenda Kiteto-Kondoa yenye urefu wa kilomita 400 kuijenga ili kupunguza msongamano wa magari mengi ya Rwanda kwenda bandari ya Daresalaam na badala yake mizigo mingi wakachukulia Tanga.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu