Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SERIKALI imetenga jumla ya Sh. Bilioni 15.5katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Taasisi ya Elimu ya Watu wazima (TEWW).
Hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.2 kulinganisha na bajeti iliyopita iliyokuwa Sh. Bilioni 14.4, katika bajeti ya 2022/2023 Sh. Billioni 11.1 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, mishahara ni Sh. Bilioni 5.8 na matumizi mengineyo ya uendeshaji ni sh. Bilioni 5.2.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini hapa. Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Michael Ng’umbi alisema katika utekelezaji wa shughuri mbalimbali Taaasisi hiyo iliandaa na kuendesha mafunzo katika kampasi zake tatu za Dar es salaam, Morogoro na Mwanza.
‘’Katika mwaka wa fedha 2022/2023TEWW itaendelea kutekeleza majukumu yake katika eneo hili ikiwa ni pamoja na kuwatumia wanachuo wake katika kufungua vituo kisomo nchi nzima’’, alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha Dkt. Ng’umbi program tatuza mafunzo zilitolewa kwa njia ujifunzaji wa kawaida na kwa njia ujifunzajia huria na masafa,ambazo ni elimu ya watu wazima na mafunzo endelezi.
Alizitaja nyingine kuwa ni Elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii na Elimu ya Masafa kwa ngazi ya Astashahad,Stashahada na Shahada.
Aidha katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Dkt. Ng’umbi alisema TEWW inaendelea na utekelezaji wa jukumu hili ikiwa pamoja kukamilisha mtaala wa mafunzo ya walimu wa elimu ya watu wazima katika maeneo ya Ufundi na teknolojia.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 TEWW ilipokea maombi 62 kutoka kwa wadau wakiomba usajili wa kuendesha vituo vya shule huria za Sekondari Tanzania Bara hata nhivyo waombaji 58 ndio waliokidhi vigezo na kusajiliwa.
‘’Katika mwa huu fedha TEWW itaendelea kuboresha nyenzo za usimamizi wa utoaji wa elimu nje ya mfumo rasmi katika ngazi ya elimu ya Msingi ili kuhakikisha ubora wa mafunzo unatolewa na vituo vilivyosajiliwa’’, alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha Dkt. Ng’umbi alisema katika mwaka wa fedha uliopita TEWW ilifanikiwa kuanzisha madarasa 406 ya kisomo (Kusoma,kuandika,kuhesabu pamoja na mafunzo ya ujuzi), ambapo madarasa hayo yalikufunguliwa katika shule zaMsingi za umma katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
‘’Madarasa hayo yamenufaisha jumla ya wanakisomo 5777 na yamekuwa yakitumika kama vituo vya mafunzo kwa vitendo na utafiti kwa walimu wanafunzi wa TEWW’’, alisema Dkt. Ng’umbi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa