Na Kija Elias,TimesMajira Online,Moshi
SERIKALI imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 14.722 kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara mkoani Kilimanjaro.
Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Motta Kyando, ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara.
Amesema Wakala wa barabara mkoa wa Kilimanjaro iliingia mikataba 32 na wakandarasi kwa ajili ya shughuli za matengenezo ya barabara.
Amesena Serikali ilitenga bajeti ya miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 12.073 kati ya hizo shilingi bilioni 1.6 zimetoka mfuko wa barabara na shilingi bilioni 10.5 serikali kuu.
Kyando amesema tayari wakala wa barabara umepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.05 sawa na asilimia 871 kwa ajili ya kufanya shughuli za miradi hiyo ya maendeleo.
“Wakala wa barabara tayari tumekwisha kupokea fedha za maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 11.6 sawa na asilimia 78.5 za matengenezo,”alisema Kyando.
Aliongeza”Utekelezaji wa matengenezo hadi sasa ni asilimia 77.9 ambapo tayari wakandarasi wamekwisha lipwa asilimia 41 ya fedha tulizozipokea,”alisema.
Mhandisi Kyando amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara.
“Katika fedha hizo kutakuwa na matengenezo ya kawaida, matengenezo maalum, matengenezo ya madaraja, pamoja na matengenezo makubwa,”amesema.
Hata hivyo Kyando amesema Serikali pia imetenga kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo katika hiyo wanayo miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani hadi Mkomazi ywnye urefu wa kilometa 6.5.
Aidha amesema Wakala wa barabara mkoa wa Kilimanjaro unaendelea na ukarabati wa uwanja wa ndege Moshi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami na changarawe.
“Tunayo pia miradi ya Kitaifa ya barabara ya Bomang’ombe-Sanya Juu hadi Kamwanga yenye urefu wa kilometa 25 ambapo barabara hii ukarabati mkubwa ni kilometa 74 kwa kiwango cha lami,”amesema.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi