Na Joyce Kasiki,Dodoma
SERIKALI imeupongeza uongozi wa Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa jitihada wanazozifanya kwa maendeleo ya Chuo hicho na Taifa kwa ujumla huku ikisema ipo tayari kushirikiana na chuo hicho ili kuhakikisha kinakuwa na mazingira Bora ya kazi na kujifunzia.
Hayo yamesemwa leo Novemba 23,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mipango, Wizara ya Fedha Moses Wilson katika Kongamano la kitaaluma la IRDP kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo .
“Ninatambua Bado mna uhitaji wa mabweni ,miundombinu zaidi kwa ajili ya kuongeza idadi kubwa zaidi ya wanafunzi ,na ujumbe huu nitaufikisha kwa Waziri wa Fedha na ninaamini kwa pamoja tutafikia matarajio yenu.”amesema Wilson na kuongeza kuwa
“Napenda kuupongeza uongozi wa Chuo Cha Mipango kwa mafanikio makubwa ya chuo hicho tangu kiliposajiliwa mpaka sasa.”
Awali Mkuu wa Chuo hicho Hozen Mayaya ameelezea mafanikio ya Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kutoka 23 na wafanyakazi 14 mwaka 1979 hadi kufikia wafanyakazi 400 na wanafunzi zaidi ya 14,000.
Vile vile amesema walianza kutumia Ofisi katika majengo ya kupanga lakini sasa wanatumia majengo waliyojenga wenyewe huku akisema wana majengo ya kisasa ambayo yanavutia katika kufanya kazi na hata wanafunzi kujifunza .
Doricas Samson mwanafunzi ambaye pia ni mjasiriamali anayejishughulisha na uongezaji thamani wa bidhaa za chakula lakini pia ni mmoja wa wanafunzi walio katika kikundi cha Mipango Interprenureship organization center amekishukuru Chuo hicho kwa kuwajengea uwezo wa kujiajiri.
Amesema Chuo hicho kinatoa fursa Kwa wanafunzi kujiandaa kujiajiri na hivyo kukabiliana na soko la ajira hasa kwa vijana hapa nchini.
Naye Thabita Mbando mwanafunzi wa Chuo hicho ambaye ni mhitimu wa ngazi ya Diploma anajihusisha na utengenezaji wa bidhaa za ubuyu ambapo amebuni bidhaa ya jam ya mkate kwa kutumia ubuyu.
“Na hii ni kutokana na namna chuo kinavyowalea wanafunzi na kutufundisha Ili kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa na uwezo wa kujiajiri badala ya kutegemea ajira za Serikali. “amesema Thabita
Ameiomba Serikali iendelee kiwasapoti wanafunzi na wajasiriamali wengine waliopp nchini Ili kuhakikisha jamii inakuwa na uwezo wa kiuchumi na hivyo kuchangia katika Pato la Taifa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi