Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Imeelezwa kuwa serikali,imeweka mazingira rafiki,bora na saidizi ya uwekezaji yenye lengo la kuinua uchumi wa Tanzania pamoja na kuwapatia maendeleo wawekezaji ndani ya jamii.
Hayo yameelezwa Septemba 4, 2024 jijini Dar-es-Salaam na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Hanspaul, Satbir Singh Hanspaul.Ambapo ameipongeza serikali kwa kuwawekea mazingira saidizi,ambayo ni rafiki kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uzalishaji hapa nchini.
Pia Hanspaul amewasisitiza Wakandarasi wenzake, kutumia fursa hiyo kufanya kazi, huku wakifuata maagizo, sera na maelekezo ambayo ni rafiki kwa wawekezaji wazawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chemba ya sekta ya Uchukuzi ya Miundombinu Tanzania, Steven Mkomwa, ameeleza kuwa mkutano huo umewafunza mambo muhimu ikiwemo kulipa kodi na kutumia rasilimali watu wazawa kwenye maeneo yao.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote