December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaonya wizi,udanganyifu wa mtihani darasa la Saba

Na Joyce Kasiki,Timesmajira,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia amekea vitendo vya wizi na udanganyifu wa mitihani ya darasa la Saba inayotarajiwa kuanza kesho nchini kote.

 Aidha amewatakia wanafunzi wote Kila la kheri na kuwataka walimu na wazazi kuwapa watoto sapoti katika kipindi hiki muhimu Ili waweze kufanya vizuri kwenye mtihani wao wa kuhitimu darasa la Saba.      Aidha amewataka walimu na wasimamizi wote wa mitihani kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu huku akisema wale wenye ñia ya kutaka kufanya udanganyifu waache mara moja.

Amewataka wanafunzi kutambua kwamba wanaofanya udanganyifu au kufanya udanganyifu ni athari na madhara yake ni makubwa sana katika maisha yao kwa ujumla. 

“Licha ya kwamba sasa Hali imekuwa nzuri sana kutokana na udanganyifu na wizi wa mitihani kupungua lakini  tunaendelea kulikemea suala hilo,udanganyifu wa mitihani katika mtihani na hasa ule wa kuandaliwa na walimu,wenye shule au maafisa wa Serikali unakwaza sana mfumo wetu wa Elimu  ,kwanza hatuwatendei haki wale wanaofanya mtihani bila kuibia kwa sababu mwanafunzi anaweza kufaulu kwa sababu tu kaonyeshwa mtihani kwa hiyo unamdhulumu yule ambaye hakuonunyeshwa mtihani  lakini pia ni kinyume Cha desturi zetu .”amesema Prof.Mkenda

Ameongeza kuwa “Pamoja na hayo ukimfundisha mwanafunzi kwamba unaweza kuibia Ili ufaulu unamfundisha rushwa na wizi mapema sana lakini pia tu anaharibu weledi katika mfumo wetu wote hapa nchini,maana hawa wanafunzi wengine watakuwa madaktari na wengine watakuwa kwenye mifumo yetu nyeti na madhara katika jamii na mfumo wetu yatakuwa ni makubwa sana ,kwa hiyo nahimiza tena sote na hasa maafisa wa Serikali ,maafisa Elimu na kamati za mitihani kuanzia shule wote tufungue macho yetu kuhakikisha kwamba hakuna wizi wa mitihani ,

“Na narudia tena kwamba popote atakapobainika afisa wa Serikali au mwalimu  kujihusisha kwa namna yoyote ile na udanganyifu wa mitihani tutahakikisha kwamba anafukuzwa kazi na anashitakiwa.

Prof.Mkenda ametumia nafasi hiyo kutaja  namba zitakazowawezesha wananchi  kutoa taarifa za viashiria vya wizi wa mitihani kuwa ni 0759360000 huku akisema taarifa hiyo itakuwa ya siri