Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Arusha
SERIKALI imeombwa kuangalia namna ya kuwabadilishia mitaala Kwa wanafunzi wenye ulemavu kulingana na aina ya ulemavu walio nao.
Kwani kwa sasa mitaala iliopo ni ya wanafunzi wote mara nyingine unasababisha changamoto kwa watoto wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na Gabriel Mhemela ambaye ni Makamu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Holly ghost inclusive iliopo Tengeru Wilayani Meru mkoani Arusha wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mitaala hiyo.
Amesema mtaaala uliopo ni mzuri sana kwa watoto Ambao hawana ulemavu lakini Kwa wenye ulemavu wakati mwingine huwa unasababisha washindwe kuelewa vyema.
“Mtaala Una mambo mengi sana na maelezo mengi sana sasa unakuta mtoto au mwanafunzi mlemavu ana changamoto nyingine hii inasababisha aelewe Kwa shida Sana wakati angekuwa na mitaala yake wangeelewa haraka Sana”amesema.
Pamoja na hayo Mhemela aliitaka jamii kuhakikisha kuwa na wao wanajifunza lugha za alama Kwa walemavu ili iwe rahisi kwao kupata mahitaji na misaada hasa wanapoitajika.
“Tunatoa rai Kwa watanzania sasa kuhakikisha kuwa wanajifunza lugha hizi za alama ili pindi anapotokea mtoto au mlemavu kwenye jamii aweze kupata haki zake za msingi kwani walemavu nao Wana Haki zote kama binadamu,”amesema.

Akiongelea programu maalumu za kuwaongezea ujuzi watoto hasa wenye ulemavu shuleni hapo amesema kuwa wanapata utaalamu mbalimbali hasa wa stadi za maisha.
“Kwa shule yetu hapa wanajifunza mambo mbalimbali mfano mzuri kuna ambao wanatusaida kutengeneza mikate wakati wengine wakiwa wanajifunza kushona na hii inawasaidia hata huko mbeleni kuweza kujiajiri.
Alihitimisha kwa kuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaendelea kushirikiana na shule hiyo ya viziwi ikiwa ni pamoja na kuwapa watoto wote haki ya kupata elimu hasa kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi