Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online
Ubora wa Benki ya NMB kiutendaji miaka ya hivi karibuni na mafanikio yake makubwa kifedha mwaka jana ni miongoni mwa matokea ya ubunifu na uwekezaji katika mifumo ya kisasa hasa ile ya kidijitali.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna wakati akizungumza Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Amesema mifumo hiyo imekuwa na tija kubwa si tu kwa taasisi hiyo kinara wa faida, bali pia kwa Serikali, wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018, serikali imeweza kukusanya mapato yenye thamani yatakribani sh. trilioni 6 kupitia mifumo hii ambayo pia ina mchango mkubwa kwenye ufanisi wa NMB kifedha.
Ruth amesema hayo kabla ya kumkabidhi DktMpango hundi ya sh. bilioni 21.8 ambazo NMB imezitoa kwa Serikali kama gawio la mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la asilimia 43 ya kiasi ilichokitoa mwaka 2019.
Aidha, pamoja na kuwa mwanahisa mkubwa kwenye benki hiyo, pia serikali ni mteja mzuri na mdau wa kimkakati wa NMB kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Pamoja na miradi hii, uwekezaji ambao Benki ya NMB imeufanya kwenye teknolojia, unaendelea kuiwezesha benki kuunganisha mifumo yake na taasisi mbalimbaliza serikali na zisizo za kiserikali na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa mapato,” amesema Zaipuna.
“Serikali, zaidi ya kuwa mbia, ni mteja mzuri na mkubwawa Benki ya NMB. Sisi tunalitambua hilo natumeendelea kuwekeza katika teknolojia inayotoa suluhisho kwa Serikali,” amefafanua.
“Pamoja na kuunganisha mfumo wa malipo ya serikalikatika mifumo ya Benki ya NMB, tunaendelea kuwekeza kuhakikisha miamala mingine mbalimbali inafanyika kwa njia ya kielekroniki,” amesema na kuongeza;
“Juhudi hizi zote zinachangia kuleta ufanisi na pia kupunguza gharama za uendeshaji katika ukusanyaji wamapato. Kwa miaka mitatu, 2018/20, jumla ya sh. trilioni 5.9 zimekusanywa kupitia mifumo ya Benki ya NMB ambayo imeunganishwa na taasisi mbalimbali zilizopo nchini.”
Mbali na malipo ya gawio, ambalo katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 yamefikia sh. bilioni 155.8, Dkt Mpango amesema NMB kuiwezesha serikali kukusanya mapato kupitia mifumo yake ni mchango mwingine mkubwa ckutoka benki hiyo mahili.
Alisema serikali inajivunia mafanikio makubwa ya NMB na kuwa mbia kwenye taasisi hiyo kitu ambacho kinaifanya kupata faida nyingi zenye tija kutokana na uwekezaji wake wa asilimia 31.8. Dkt. Mpango aliwachagiza Watanzania kuhakikisha benki hiyo inazidi kuwa imara kwani faida zake ni kubwa kwao na taifa kwa ujumla.
“Tunajivunia uwekezaji wetu katika NMB kwani unalipa. Serikali kwa niaba ya wananchi tunaipongeza NMB kwa kazi inazozifanya kuwahudunmia Watanzania na uchumiwa taifa kwa ujumla,” amefafanua Dkt Mpango.
Katika kipindi cha miaka mitano, benki hiyo imeweza kuukuza mtaji wa wanahisa wake kwa ongezeko la zaidi ya sh. bilioni 463, hivyo kuufanya mtaji wake kufikiaTZS trilioni 1.1 ukilinganisha na TZS bilioni 666 mnamomwaka 2015.
Pia NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia ajenda yakitaifa ya kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania. Zaipuna alisema wigo mpana wa bidhaa na huduma zake umeongeza upatikanaji wa suluhisho za kifedha kupitia njia za kawaida na njia mbadala za kibenki.
Mpaka Desemba ya mwaka 2020, Benki ya NMB ilikuwa na akaunti za wateja zaidi ya milioni nne na mawakala zaidi ya 8,400 waliotapakaa nchi nzima.
“Pia tunaendelea kujikita katika uwekezaji kwenye mifumo ya kidijitali ili kuwasaidia Watanzania waliowengi kupata huduma zetu kwa urahisi, unafuu na haraka,” Zaipuna alimwambia Makamu wa Rais.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede, alisema zaidi ya ubunifu wa kidijitali, siri kubwa ya mafanikio ni wafanyakazi ambao ndiyo siraha kubwa ya benki hiyo. Aidha, mchango mwingine unatokana na ushirikiano kutoka kwa wateja pamoja namazingira wezesha ya biashara.
More Stories
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi