December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Fabian Yinza akikabidhi zawadi ya ng'ombe kwa mzazi ambaye mtoto wake alipata daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne 2019. (Picha na Mutta Robert).

Serikali yakemea mila kandamizi kwa watoto wa kike

Na Mutta Robert,TimesMajira Online, Geita

KAIMU Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Fabian Yinza amekemea mila na desturi za kufanya mtoto wa kike chanzo cha mapato ya familia kwa kumuozesha ili kupata mali hususani ng’ombe badala ya kumpeleka shule kupata elimu.

Amesema hayo katika hafla ya mpango wa kuboresha ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kitaifa katika wilaya hiyo ambayo ilikuwa ni kutoa zawadi kwa wanafunzi,wazazi na walimu walioshiriki katika kuchangia kupata matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka 2019.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Fabian Yinza akiwa na baadhi ya walimu wakiwa wameshikilia fedha walizopata kama zawadi kwa masomo wanayo fundisha kupata alama A. (Picha na Mutta Robert).

Amesema kuwa, katika wilaya kulikuwa na tabia ya baadhi ya wazazi kutopenda kusomesha watoto wa kike na kuamini kwamba msichana inabidi aolewe na kupata ng’ombe .

Amesema, wilaya hiyo iliibua mpango maalum wa kuinua ufaulu ulioitwa Performance Improvement Project(PIP) ambao ulianza kwa kuwapeleka wanafunzi kambini na kuhitimishwa kwa kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri,walimu pamoja na wazazi.

Mpango huo unafadhiliwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Bulyanhulu kupitia mpango wa kuhudumia jamii (CSR) wanafunzi walikaa kambi maalum kwa miezi mitatu kwa masomo maalum.

Ameongeza kuwa, mzazi ambaye mtoto wake anafanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza anapewa zawadi ya ng’ombe mmoja ili iwe motisha kwao ili waelewe kwamba hata mali inaweza kupatikana kupitia elimu pia.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’hwale, David Rwazo amesema mpango huo utakuwa endelevu kwa miaka mitano ili kuendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kitaifa.

Ameongeza kuwa, wilaya hiyo ilikuwa na historia mbaya ya kupata matokeo mabaya kwenye matokeo ya taifa, lakini baada ya mpango huo matokeo yameanza kuwa mazuri tofauti na zamani.

Kaimu Afisa mahusiano mahusiano wa Kampuni ya Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo alisema, wataendelea kushirikiana na wilaya hiyo katika kuinua kiwango cha ufaulu katika wilaya hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’hwale, David Rwazo amesema, mpango huo utakuwa endelevu kwa miaka mitano ili kuendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kitaifa.

Ameongeza kuwa, wilaya hiyo ilikuwa na historia mbaya ya kupata matokeo mabaya kwenye matokeo ya taifa, lakini baada ya mpango huo matokeo yameanza kuwa mazuri tofauti na zamani.

Kaimu Afisa mahusiano mahusiano wa Kampuni ya Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo alisema, wataendelea kushirikiana na wilaya hiyo katika kuinua kiwango cha ufaulu katika wilaya hiyo.

Aliongeza kuwa, mgodi huo ulishiriki katika mpango huo wa kuinua kiwango cha ufaulu katika wilaya hiyo kwa kununua vitabu 900 na kutoa chakula kwa ajili ya wanafunzi na walimu waliokuwa kambini kwa miezi mitatu na kununua zawadi ya ng’ombe kwa wazazi watano ambao watoto wao wamepata matokeo mazuri zaidi.

Senkondo alisema kuwa, zawadi nyingine ni fedha taslimu kwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza pointi 12 kwa 500,000 pointi 13 kwa 300,000 kwa daraja la pili ,wasichana walipata 500,000 kwa daraja la pili 200,000.

Senkondo aliwataja wengine waliopata zawadi ni walimu ambao masomo yao yalipata alama A ,shule ambazo ufaulu ulikuwa mzuri,shule ambazo ufaulu ulizingatia jinsia na wazazi watano ambao watoto wao walifaulu vizuri.

Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu Barrick Bulyanhulu imeamua kutoa motisha kwa wanafunzi,walimu na wazazi kwa kuwapongeza kwa matokeo mazuri ya kidato cha nne mwaka 2019.

Wilaya hiyo ilianzisha utaratibu huo ili kuinua kiwango cha ufaulu katika matokeo ya mitihani ya taifa ambapo wilaya hiyo ilikuwa inapata matokeo mabaya ambapo mwaka 2018 ilipata daraja la kwanza 9 na mwaka 2019 ilipata daraja la kwanza 20.