November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaitaka DART kuboresha huduma haraka

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed O. Mchengerwa ameelekeza Uongozi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuongeza watoa huduma ili kuboresha huduma ya usafiri wa haraka kwa Wananchi wa Dar es salaam.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kupata taarifa ya Utendaji kazi wa Wakala huyo leo tarehe 24.10.2023.

Amesema huduma ya Mabasi yaendayo haraka ni muhimu sana kwa maisha ya wakazi wa Dar es salaam na inatakiwa kusaidia kupunguza adha ya usafiri sasa anapokua kuwa mtoa huduma mmoja anazidiwa hivyo kusababisha changamoto kwenye baadhi ya maeneo.

Amesisitiza kuwa suala la kuongeza watoa huduma kwa sasa haliepukiki na linatakiwa kuwa kipaumbele kwanza kuna njia mpya zitakazoanza hivi karibuni hivyo akipatikana mtoa huduma mwingine wa kusaidiana na huyu aliyepo kwanza italeta ushindani na atahudumu kwenye njia mpya na hivyo kuboresha utoaji wa huduma hii ya usafiri kwa wananchi wa Dar es salaaam.

Mtoa huduma mliyenaye sasa ni mmoja tu ambaye anatoa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka anakosa ushindani wakiwa wawili ni rahisi zaidi kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi wote wanaotumia huduma hii.

“Mtoa huduma mliyenaye kwa sasa ni UDART Pekee muda umefika sasa kuwa na mtoa huduma zaidi ya mmoja ili kuleta ushindani kwenye kutoa huduma za Usafiri kwa ili wananchi wapate huduma bora amesisitiza Mchengerwa.

Pia Waziri Mchengerwa amewataka Uongozi wa DART kuimarisha mifumo ya kutoa Taarifa mara tu panapoteka changamoto yeyote ya usafiri

“Sitapenda kuendelea kuona vurugu kwenye Vituo vya kusubiria mabasi mara tu kunapotokea hitilafu kuwa na mifumo ya kutoa taarifa ili kupunguza manung’uniko ya wananchi ambao huenda wamekaa pale muda mrefu kusubiria Basi.”

Mwanzoni akitoa taarifa za Utendaji kazi wa Wakala huyo Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Edwin Mhede amesema katika kipibdi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu uwezo wa kusafirisha abiria kwa siku umeonhezeka kutoka abiria elf 90 mpaka 210,000 na hii yote ni kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika kwa Wakala huyo.