Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
SERIKALI imeipongeza Kampuni ya ukandarasi kutoka nchini China ya CRJE (East Africa) Ltd kwa ufanyaji kazi uliotukuka huku ikiahidi kuendelea kukuza mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na China Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Uwajibikaji kwa Jamii ya CRJE kwa ushirikiano na Hoteli ya Johari Rotana.
Hafla hiyo ilihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo, John Mnali, Mkurugenzi wa Ukuzaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku na balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Ndumbaro, ofisa mwandamizi katika wizara hiyo Shoma Philip Ndono, alisema Kampuni ya CRJE imeongeza kwa kiasi kikubwa uhusiano mwema wa urafiki kati ya China na Tanzania.
“Tunashukuru na tunatamani urafiki wetu uendelee kudumu kwa muda mrefu ujao.”Alisema kampuni hiyo ya ukandarasi kutoka China ipo Tanzania kwa zaidi ya miaka 55 na imefanya kazi nzuri kwa ustawi wa jamii ya Watanzania.”CRJE wamehafanya miradi zaidi ya 200 na wametoa mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa watanzania pamoja na utekelezaji wa uwajibikaji kwa jamii” alisema.
Akizungumza kando ya hafla hiyo, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa TIC John Mnali aliishukuru kampuni hiyo ya China kwa kuzindua ripoti hiyo na kuitaka kuvuka mipaka na kusaidia changamoto zinazoikabili jamii.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikisaidia jamii katika elimu, miundombinu na utunzaji wa mazingira jambo ambalo lina mchango mkubwa katika malengo ya maendeleo endelevu ya Tanzania.Mnali alisema uwazi na uwajibikaji ni msingi wa kampuni hiyo ya kutoka China akiyataka Makampuni mengine kuiga mfano ulioonyeshwa na CRJE.
Aliitaka kampuni hiyo kuendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali na taasisi nyingine kwa manufaa ya nchi ya Tanzania a China.Aliongezea kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha kuwa wawekezaji wanafanya shughuli zao chini ya mazingira mazuri.
Katika hotuba yake, Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian alisema: “Kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, napenda kutoa pongezi na shukrani zetu za dhati kwa CRJE kwa mchango wao katika uwajibikaji wa kijamii.Balozi huyo aliendelea kusema: “CRJE imefanya mengi makubwa nchini Tanzania kwa miaka 55.
Ilianzishwa mwaka 1969, ilihusika katika ujenzi wa reli kubwa ya Tazara, mradi mkubwa zaidi kwa ruzuku kutoka China.”Alibainisha miradi mingine mikubwa ambayo imefanywa na CRJE ni pamoja na ujenzi wa daraja la Nyerere, ukumbi mpya wa mijadala wa Bunge, kituo cha mikutano cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma, Nyerere Foundation Square na Shule ya Uongozi ya Nyerere. “Wameshajenga zaidi ya mita za mraba milioni 3, miradi mikubwa 200 nchini Tanzania.”
Aliongezea: “CRJE imeshatunukiwa tuzo ya mkandarasi bora wa kigeni mara tatu nchini Tanzania, na tuzo ya Luban mara tatu – Tuzo ya Oscar ya China kwa ubora katika ujenzi.” Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CRJE Jiang Yuntao alisema kuwa kuinduliwa kwa Ripoti yao ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ni hatua muhimu ya kweli katika maendeleo ya kampuni yao na ni kielelezo cha dhamira ya kufanya kazi bega kwa bega na jamii ya watanzania.Yuntao alisisitiza: “Kwa miaka mingi, tumejitolea sio tu kwa ujenzi wa miundombinu lakini pia uwekezaji, uwekezaji wa jumla ya zaidi ya dola milioni 260.”Alimalizia: “Ripoti yetu hii ya CSR haiakisi tu kazi tuliyofanya huko nyuma bali pia ni ahadi ya kuendelea kuchangia ukuaji na maendelea kwa nchi ya Tanzania. Tumejitolea kufanya kazi kwa karibu na serikali ya Tanzania, sekta binafsi, na jumuiya za mitaa ili kusaidia maendeleo ya taifa na kuboresha ubora wa maisha kwa watanzania.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi