Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Serikali yaeleza mikakati ya nchi katika kudhibiti ugonjwa wa Kifua kikuu na Ukoma ifikapo 2025 .
Hayo yalisemwa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt ,Mbarouk Seif, wakati wa mafunzo kuhusu huduma za Kifua kikuu kwa waandishi wa Habari wa Dar es Salaam.
Dkt ,Mbarouk alisema katika malengo hayo mikakati walioweka Serikali ni kupunguza mambukizi mapya ya kifua kikuu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 ikilinganishwa na mwaka 2015
“Mikakati ya Serikali kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2025 ikilinganishwa na hali ya mwaka 2015 pamoja na kupunguza Ulemavu unatokanao na Ukoma kwa asilimia
90″alisema Dkt.Mbarouk
Dkt ,Mbarouk alisema katika Mikakati hiyo ya kukabiliana maambukizi hayo vipaumbele vya nchi katika utekelezaji wa mpango mkakati kuwafikia watu wote ambao hawajagundulika
kuwa na Kifua Kikuu na kuwaweka kwenye matibabu .
Aidha alisema pia kuboresha teknolojia za upimaji kuhusisha watoa huduma katika vituo binafsi yakiwemo maduka ya Dawa na kushirikisha Jamii’ na watoa huduma katika ngazi ya Jamii’
Pia alisema Mikakati mingine vipaumbele vya nchi katika utekelezaji wa mpango mkakati huo ushirikishwaji Jamii’ na Sekta binafsi ,kama vile vituo binafsi vya afya na maduka ya Dawa Pamoja na Waganga wa Tiba asili kuibua wagonjwa wa kifua Kikuu.
Mratibu wa TB Tanzania STOP TB Partnership Muungano wa wadau wa kupambana na Kifua kikuu Tanzania Nelson Telekela , alisema maadhimisho ya Kifua Kikuu yanatarajia kufanyika Mkoa wa Simiyu Mwaka huu Machi 24 Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, na Kaulimbiu ya siku ya Kifua Kikuu mwaka huu 2023 “Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Kifua Kikuu nchini Tanzania.
Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wilaya ya Mnazi Mmoja Dkt.Linda Mutasa ,alisema Kifua kikuu sio ugonjwa wa Kulogwa bali ni ugonjwa sugu wa kuambukiza na kuenezwa kwa njia ya hewa pindi mgonjwa asiyeanza matibabu anapokohoa au kupiga chafya ,hakuna uhuaiano wowote na Kulogwa .
Dkt.Linda alisema Kifua kikuu sio ugonjwa wa kurithi ,bali ugonjwa huo huweza kuwapata wanafamilia au Jamii ambayo wanaishi pamoja kama kuna mgonjwa ambaye bado hajaanza matibabu hivyo kupelekea wanafamilia hao baadae kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi