January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

serikali ya Mtaa Machimbo Segerea wapewa viti

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Kikundi cha Wanawake wa Mtaa wa Machimbo kata ya Segerea ,wamemzawadia viti Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Machimbo Segerea, Mariam Machicha kwa ajili ya Serikali ya mtaa vitumike katika shughuli za kijamii na mkutano.

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Machimbo Mariam Machicha , alipokea viti hivyo ofisi ya Serikali za mitaa Agosti 15/2024 ambapo aliwashukuru wanawake wa mtaa huo kwa ushirikiano wao.

“Nawapongeza wanawake wa kijiji cha Machimbo kwa umoja wao kuisaidia Serikali yao ya Mtaa ,ofisi yetu ya Mtaa itawapa ushirikiano katika umoja wao kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi waweze kusonga mbele kuisaidia chama na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Machicha.

Mwenyekiti Mariam Machicha ,alisema kikundi hicho cha wanawake wa Mtaa huo ni cha shida na raha msaada huo wa viti walivyotoa ni sehemu ya kusaidia serikali katika huduma za jamii .

Aidha Mariam Machicha alisema kwa niaba ya Serikali ya Mtaa na Wajumbe wake wanawashukuru na kuwapongeza kwa kushiriki shughuli za kijamii kuisaidia Serikali

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa kijiji cha mtaa wa Machimbo EMMY MGOTA alishukuru Serikali ya Mtaa huo kwa utendaji bora wa kazi na kuwapa ushirikiano Kikundi hicho kufikia mafanikio yao na malengo ya kukuza biashara.

Mwenyekiti wa Wanawake wa Kijiji cha Mtaa wa Machimbo kata ya Segerea EMMY MGOTA alisema kikundi Chao cha kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya kusaidiana WANAWAKE jamii inayowazuunguka kinashughulika kukodisha viti katika mikutano,misiba katika Sherehe mbali mbali, kwa kuchangia kiasi cha pesa kidogo.

AFISA MTENDAJI wa Mtaa wa Machimbo kata ya Segerea Isdory Sumuni ,ametoa shukrani kwa kikundi cha Wanawake wa mtaa Machimbo Segerea.

AFISA Mtendaji wa mtaa wa Machimbo Segerea Isdory Sumuni aliwataka vikundi vingine kuiga mfano wa Wanawake wa Machimbo Segerea walivyosaidia Serikali yao ya Mtaa