Na Nasra Bakari,TimesMajira,Online
MKUU wa Kitengo cha Uhusiano cha Ubalozi wa Finland, Sanja Ohra
amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na janga la UVIKO_19 kwa zaidi ya asilimia 61 na pia imejidhatiti katika kupambana na rushwa kwa asilimia 61.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu huyo, amesema kulingana na ripoti ya maoni iliotolewa na Taasisi ya External Relationship Technique kutoka nchini Finland imebaini utendaji wa uongozi wa Rais Samia ni mzuri na endapo kukatokea na uchaguzi Rais Samia anaweza kushinda kwa asilimia 75.
Amesema, kwa mujibu wa ripoti ya utendaji kupitia washiriki 67 walisema serikali ya Rais Samia imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kwa zaidi ya asilimia 61 pamoja na ushirikiano mkubwa kwa vyama vingine. “Katika upande wa kusimamia haki, usawa, amani na utangamano Serikali ya Rais Samia imeweza kulinda haki na kudumisha amani kwa zaidi ya asilimia 9,”amesema na kuongeza
“Asilimia 60 ya washiriki wamesema serikali imejenga uchumi kwa zaidi ya asilimia 61 na hii imetokana na kujenga mahusiano ya kimataifa, serikali imeweza kukuza kwa zaidi ya asilimia 61, ” amesisitiza
Ohra amesema, asilimia 39 ya baadhi ya changamoto zinazowakabili watu katika maeneo mbalimbali zimeweza kufanyiwa kazi ikiwemo Sekta ya Nishati, Kiilimo,Maji,Biashara,Ardhi na Afya.
Amesema, katika ushirikiano wa mihimili ya serikali wamefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 88 na jambo linalowavutia watanzania katika uongozi wa Rais Samia ni kuendeleza miradi ya kimkakati kwa zaidi ya asilimia 61.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria