Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
SERIKALI waipongeza shule ya Sekondari ya Juhudi kwa kufanya vizuri kitaaluma na nidhamu nzuri kwa WANAFUNZI wa shule hiyoPongezi hizo zilitolewa katika mahafali ya kumi na nane ya kidato cha nne na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji Mwalimu Mussa Ally aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya Ilala Arch ,Ng’Wilabuzu LUDIGIJA katika mahafali hayo.
Akizungumza katika hotuba yake Mwalimu Mussa Ally amesema Serikali wanaipongeza shule ya Juhudi ni kati ya shule zinazofanya vizuri Kitaaluma na nidhamu na kijamii ikiwemo kuimalisha Mazingira ya shule na miundo mbinu ikiwemo walimu Wana shirikiana .
” Shule ya Sekondari ya Juhudi ni ya Kimataifa ina fanya vizuri hadi katika usimamizi wa madarasa ya UVIKO Mkuu wa shule hii alipewa zawadi kwa usimamizi mzuri wa madarasa ya Shule sipati tabu na shule ya Juhudi ” alisema Mwalimu Mussa .
Mwalimu Mussa Ally amesema kuna shule kila siku kazi yangu kutafuta walimu wasio timiza wajibu wao lakini juhudi wanaupiga mwingi katika taaluma .
Aliwataka Wanafunzi kujiandaa vyema na mitihani yao ya kidato cha nne na kutaendeleza mazuri waliofundishwa amewataka wajimalishe Kitaaluma .
Akizungumzia changamoto za shule ya Juhudi amesema atazifanyia kazi yeye ndio Mtendaji ,Halmashauri ya Jiji ina mpango wa kuboresha shule Sekondari ya Juhudi kwa kujenga gholofa Kwa Sasa wanafanya upembuzi kwa ajili ya ujenzi huo, kata ya Liwiti ,Kipunguni na Ilala pia wanajenga shule ya Sekondari ya gholofa wameshaomba kibali kwa ajili ya kujenga magolofa mjini shilingi Bilioni 6.2 Serikali imetoa kwa ajili ya madarasa 310 .
Alimtaka Mkuu wa shule ya Sekondari ya Juhudi kushirikiana na wadau katika sekta ya Elimu kwa ajili ya kuimalisha shule hiyo .
Mwalimu Mussa aliwataka WANAFUNZI kuweka malengo mazuri ya kujiendeleza wakiwa nyumbani kusubiri matokeo yao ya kujiendeleza .
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari