January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali mbioni kukamilisha mkakati wa utoaji wa huduma ya afya ya akili

Na. Catherine Sungura,WAF-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya afya inatarajia kukamilisha mkakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa afya ya akili ikiwemo afya ya akili mashuleni,kazini pamoja na kwenye jamii.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Tiba Dkt. Omary ubuguyu wakati wa mahojiano na Televisheni ya Channel Ten wakati wa kipindi cha baragumu mapema wiki hii.

Dkt. ubuguyu amesema mkakati huo unatarajia kutoka mwaka huu ambapo utajikita katika sehemu tatu ikiwemo afya ya akili mashuleni na kutaja kuwa sehemu kubwa ambayo watu wanaweza kupata shida na magonjwa mengi ya afya ya matatizo ya akili yanatokea kabla ya miaka 25.“Aidha, changamoto kubwa zitatokea hapo chini au wagonjwa wengi wataonekana kwenye umri huo”.

Kwa sehemu ya afya ya akili makazini Dkt. Ubuguyu amesema sehemu hiyo ndio inayoathiri kwa kiwango kikubwa kuliko sehemu yoyote na kuongeza kuwa sio sehemu za ajira rasmi tu bali ni sehemu yeyote ambayo watu wanapata kipato ikiwemo sokoni na kutolea mfano soko linapounguahivyo mkakati huo utaenda kuangazia eneo hilo.

Dkt. ubuguyu ametaja pia sehemu ya tatu ni afya ya akili katika jamii ambap ndio ombwe kubwa kwani taktika jamii unapotaja afya ya akili watu huanza kucheka na kuona magonjwa au shida mbele badala ya kuonekana afya kwa ujumla wake kwani watu wanapowasiliana ni kwamba afya zao za akili zipo sawa.

Hata hivyo Dkt. Ubuguyu amesema suala la afya ya akili Wizara ya afya imelipa kipaumbele ikiwemo maboresho ya miundombinu kwenye hospitali ya Taifa ya afya ya Akili ya Mirembe pamoja na hospitali za rufaa za mikoa.

“Uwekezaji katika miundombinu na kwa watoa huduma ambapo hivi sasa tumefanyia maboresho makubwa kwenye Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe hospitali za rufaa za mikoa 11 kati ya 28 zinatoa huduma za afya ya akili hasa huduma za kulaza”.Amesema

Kwa upande kwa kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ni utoaji wa elimu kwa ujumla kwa maana watu waelewe kuhusiana na masuala ya afya ya akili na si kusubiri kushughulika na watu wenye Magonjwa ya akili.

Ameongeza kuwa Wizara ya Afya inayo jukumu kubwa la kushughulikia afya ya akili pamoja na Wizara ya maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ambayo inashughulikia na afya ya akili aidha, inayo watu wenye makundi maalumu hivyo kuhakikisha watu hao hawapati changamoto za afya ya akili

Changamoto ya afya ya akili Kitaifa Dkt. Ubuguyu alisema hali ni mbaya na sio tu Tanzania bali dunia nzima na kuongeza kuwa sehemu kubwa ya ukatili imebebwa na sehemu ya malezi kuanzia kwa watoto ambapo makuzi yanakuwa sio mazuri kwani wazazi wamekubwa ‘busy’ kutafuta maisha na hali ya kuchangamana na watu ikiwemo mitandao ya kijamii.

“Uchochoe wa vurugu na matatizo kwenye jamii ni ukorofi pamoja wazazi wengi huelekeza watoto kwa kupiga hivyo ukatili huo humfanya mtoto kujua hayo ndio maisha na hivyo inakua rahisi kuwa na ukatili kwa jamii tofauti na zamani ambapo watoto walikua wakipelekwa kwa babu na bibi zao”.

Dkt. Ubuguyu ametoa wito wa jamii na familia kwa ujumla kuacha tabia ya ukatili kwa watoto na hivyo kujenga mazoea ya kukaa na kuongea pamoja kama familia kwani dunia imebadilika.