December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kuunda kamati kukabili COVID 19

Na Aveline Kitomary, TimesMajira Online,Dar es Salaam.

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaunda upya kamati maalum  kwaali ya kuchunguza ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid 19)  ili kuweza kushauri serikali nini cha kufanya.

Rais Samia aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu katibu wakuu. wa Wizara  na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali

“Suala la Covid -19 nafikiria niunde kamati ya wataalamu waliangalie  kwa upanda wake kitaalamu halafu watushauri serikali ,haifai kulinyamazia aidha  kulikataa au kulikubali  bila kufanya tafiti  za kitaalamu .

“Kamati ya wataalamu kuhusu Covid -19 watuambie kitaalamu  hayo yanayopendekezwa  na ulimwengu  kuja kwwetu yapoje, hatuwezi kujitenga kama kisiwa na tutachunguza tunachoambiwa lazima tuchunguze,.

“ Rais kikwete alisema akili za kuambiwa changanya na zako hatutasikia tu ya nje tutaangalia na sisi  tuweke zetu  na msimamo maalum unaoeleweka ,sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 ulimwnguni ,tueleweka kama tunakubali au tunakataa,”amesema Rais Samia.