January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kutowavumilia wanaopotosha zoezi la uhamaji kwa hiari

Na Sophia Fundi, Timesmajira Online,Karatu

Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki amesema serikali haitawavumulia wale wote wanaopotosha zoezi la uhamaji wa hiari kwa wananchi waliojiandikisha wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kupisha uhifadhi.

Huku akieleza kuwa katika awamu ya pili ya uhamishwaji wa wananchi wanaohama kwa hiari yao serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga nyumba takribani 500 katika maeneo ya Wilaya za Simanjiro,Msomera na Kilindi.

Akizungumza katika hafla ya uvishwaji wa cheo na uapisho wa Kamishna wa Uhifadhi wa eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Richard Kiiza Waziri Kairuki amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Raymond Mwangala kwa kushirikiana na Kamshna na menejmet ya mamlaka kuhakikisha zoezi la uhamaji kwa hiari halipotoshwi na mtu yeyote na atakayebainika kufanya hivyo achukuliwe hatua kali za kisheria.

Kairuki pia amemuelekeza Kamishna na menejment kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo kuanzia uelimishwaji,uandikishaji hadi uhamishwaji kwa wale wananchi waliotayari kuhama kwa hiari kadri nyumba zitakavyokamilika.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Esta Ndungumaro amesema kuwa bodi hiyo itaendelea kusimamia mamlaka hiyo kutekeleza maagizo ya Wizara.

Akizungumza baada ya uapisho Kamishna wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Richard Kiiza amemhakikishia Waziri kutimiza wajibu wake kama alivyoapa huku akimshukuru Rais Samia kwa kumamini na kumteua.

Hafla hiyo ya uvishwaji wa cheo na uapisho ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka Wilaya ya Karatu na Ngorongoro.