July 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kushirikiana na wadau kuwawezesha vijana nchini

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

SERIKALI imesema kuwa  itaendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo katika kuwawezesha vijana kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa nchini ili kuongeza ushiriki wa vijana katika Maendeleo endelevu ya taifa.

Akizungumza jana jijini Dar Salaam, Kiongozi wa Progrya Kujenga Kesho Bora kutoka Wizara ya Kilimo( BBT),Vumilia Zikankuba wakati akizungumzia Kongamano la Vijana wanaofanya shughuli za Kilimo nchini linalotarajia kufanyika Julai 5 mwaka huu.

Zikankuba amesema miradi ya maendeleo imekuwa ikiwagusa vijana wa kitanzania bila kujali tofauti za elimu.

”Vijana wanaotakiwa katika programu ya BBT kwanza anapaswa kuwa mtanzania,awe na miaka 18  hadi 40 hatuangalii kiwango cha elimu ila mtu akijiona kuwa anaweza kufanya kilimo biashara sisi tunamchukua,”amesema

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi inayojitolea kuweka Wakulima Wadogo katika Kitovu cha Uchumi Barani Afrika,Vianey Rweyendela amesema kongamano hilo limelenga kuwakutanisha vijana hususan wale waliojikita katika masuala ya kilimo.

Amesema pia kongamano hilo linaongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kutambua mahitaji yao ili kupanua wigo wa ajira nchini.

Mmoja wa Vijana kutoka Shirika la vijana la Tanzania Youth Coalition,Josephina Onesmo amewata vijana kutumia fursa katika kuonyesha mafanikio na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika sekta ya kilimo ili kuweza kupatiwa ufumbuzi.