Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar
Mkuu wa Mkoa Dar-es-Salaam Albert Chalamila,amesema Serikali inapeleka kiasi cha milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Saranga Jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Saranga, Chalamila,amesema fedha hizo zitatolewa Ijumaa ya wiki ijayo(Aprili 18,2025),kwa ajili ya kuanza ujenzi ambao itasaidia wananchi kupata huduma karibu.

“Kilio chetu cha kwenda mbali kufuata huduma za afya Serikali imekipokea, fedha zitatolewa ili ujenzi uanze mara moja, kituo hicho kikikamilika kitatoa huduma zote zikiwemo za mama na mtoto,”amesema Chalamila.
Chalamila amesema dhumuni la ziara yake ni kutatua kero za Wananchi katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo barabara, sekta ya elimu na huduma za afya.
Katika mkutano huo, Chalamila amepata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa Wananchi, zikiwemo changamoto ya ubovu wa barabara, matatizo yanayohusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), upatikanaji wa maji safi, na ucheleweshwaji wa kukamilika kwa ujenzi wa zahanati katika eneo hilo.

Hata hivyo, Chalamila,baadhi ya kero amezitolea majibu papo hapo na kutoa maelekezo kwa viongozi husika kushughulikia changamoto hizo kwa haraka.
Pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na Serikali katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta tija.Huku akiwataka viongozi wa mitaa kuwa karibu na wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango na kwa wakati

More Stories
Waziri Mavunde azindua taarifa ya uchambuzi uongezaji thamani madini muhimu nchini
Mdiwani Bumbuli wataka jitihada ziongezwe ukusanyaji mapato
Mke wa Rais wa Msumbiji,Gueta atembelea JKCI