Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SERIKALI imesema,inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wabunifu wananufaika na kazi zao pamoja na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao katika ofisi za Hakimiliki Nchini (COSOTA) .
Hayo yamesemwa na Waziri Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Pindi Chana wakati wa semina kwa wabunge kuhus majukumu na fursa zilizopo katika ofisi hiyo ikiwemo kulinda hakimilii za wabunifu.
“Ni jukumu la Serikali kuhakikisha Sekta ya Ubunifu nchini inakua siku hadi siku, na ndio maana Serikali inandelea kuhakikisha Wabunifu wananufaika na kazi zao ,lakini pia inawaelimisha kuhusu umuhimu wa kusajili kazi zao katika ofisi yetu ya COSOTA”amesema Dkt.Chana.
Waziri huyo amesema,lengo la semina hiyo kwa wabunge ni kueleza fursa za kibiashara zilizopo katika Hakimiliki pamoja na kuongeza uelewa kuhusu taasisi hiyo kwa wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa ofisi hiyo Doreen Sinare amesema moja ya jukumu la Ofisi yake ni kuhakikisha Wabunifu wananufaika na kazi zao ikiwemo kupata mirabaha kutokana na matumizi mbalimbali ya kazi hizo.
Akitoa mada katika semina hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Miliki Bunifu la Kikanda la Afrika (ARIPO) Flora Mpanju alieleza umuhimu wa kusajili Bunifu ARIPO na nchi Wanachama kulipa ada yake.
“Zipo faida mbalimbali ambazo nchi inapata kupitia bunifu zake na kusaidia kukuza uchumi wa taifa.”amesema Doreen
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Prof. Kitila Mkumbo alisisitiza Serikali kukamilisha mchakato wa kusaini Itifaki ya Arusha kwani imechukua muda mrefu.
“Jambo hilo ni la msingi kwani litasaidia kuitangaza nchi na kukuza ubunifu katika eneo la kilimo.”amesisistiza Prof.Mkumbo
Kwa upande wa wadau wa uzalishaji wa maudhui ya Televisheni Mwasiti Badi kutoka Azam Media na Johnson Mshana kutoka DSTV, waliwaomba Wabunge hao kusaidia kukemea vitendo vya wizi wa maudhui skwa kuwa kitendo hicho kinapoteza mapato ya Serikali na kunadhoofisha uwekezaji uliofanywa na makampuni hayo.
Meneja Mkoa Ziiki Media Camila Owora ameungumzia kuhusu elimu ambapo aliwaasa wabunge kutoa elimu ya hakimiliki kwa wingi kwa wasanii na kuelewesha kuhusu kuzingatia mikataba huku akisema hiyo ni changamoto kubwa wanayokutana nayo kwa Wasanii wa Tanzania.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam