Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Licha ya ongezeko la wananchi Kata ya Buhongwa inayosababisha uhaba wa maji serikali imejipanga kuendelea kutatua changamoto hiyo kupitia mipango ya miradi mbalimbali ikiwemo ya muda mfupi,wa kati na mrefu.
Mwaka 2012 Wakazi wa Buhongwa walikuwa 26,000 na mtu wa mwisho mwaka 2017 alikuwa anapata maji kule mtaa wa Kigoto,Bulale mwaka 2018 mtu wa mwisho aliyeunganishiwa maji alikuwa na uwezo wa kupata maji, yakikatika ni masaa mawili baadae yanarejea lakini sasa kuna wakazi 75,000.
Akizungumza Julaii 27,2024 na wananchi wa Kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya Buhongwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew, amesema wanatambua changamoto ya hupatikani wa maji Buhongwa ambapo tenki lililopo Sahwa lina uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 2 huku mahitaji ni lita milioni 7.5.
“Ni ukweli usiopingika kwamba Mwenyezi Mungu ametubariki wanabuhongwa eneo letu limekuwa kivutio cha watu kujenga makazi, kufanya biashara pia ametujalia afya njema tunaendelea kuzaliana,ndio maana mpaka sasa tumefikia wakazi 75,000, sawa na chakula ambacho ulikuwa unapika kwa ajili ya wanafamilia watano,sasa wamefikia wanafamilia 15, usitegemee chakula kile kile kitaweza kuwahudumia,utaongeza unga,maji kuna endana na kuongeza bajeti,itategemea kama utakuwa umejipanga na hiyo bajeti lakini kama ujajipanga matokeo yake watu watakula chakula wengine hawata shiba,”
Ameeleza kuwa baada ya kugundua ongezeko la wananchi ndani ya Kata hiyo wamekuja na mipango mitatu ikiwemo ya mradi wa milioni 600 wa haraka utakaonufaisha mtaa wa Kigoto na Bulale,mpango wa milioni 884 pamoja na WA bilioni 1.8.
Pia amesema mpango wa muda mrefu ni mradi wa bilioni 49.9 ambao utasaidia wananchi wa Buhongwa na Misungwi utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji zaidi ya milioni 144 na utatoa maji kwa siku zote saba ukitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.
“Sasa wanabuhongwa watakaaje kwa miezi hiyo bila maji,nimetoka maelekezo tuwe na mpango wa dharura ili ndani ya miezi miwili watu waanze kupata maji,hii ni mipango midogo midogo ambayo wakati tunasubilia ule wa muda mrefu wa bilioni 49.9 kukamilika ,hii ikamilike ili watu waweze kapata maji angalau mara mbili au tatu kwa wiki,”ameeleza Mhandisi Kundo.
Hata hivyo ameahidi kuwa bomba la milimita 300 kutoka tenki la Sahwa linaunganishwa ndani ya miezi miwili litakuwa limeisha kamilika kwani wameisha fanya makadirio na kuangalia kazi iliopo hivyo kupeleka maji kwa watu wa Kigoto, Bulale na mitaa mingine.
Awali wakiwasilisha malalamiko yao mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew,baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa wameomba kutatuliwa changamoto hiyo.
“Nathubutu kumuacha mme wangu saa kumi alfajili naenda kutafuta maji,nakutana na vibaka,tutavunja ndoa zetu kwa ajili ya maji naomba mtusaidie wanawake tupate maji kwani tunateseka,”ameeleza Reaminda Wakuganda.
Naye Marry Edward ameomba mabomba makubwa yasambazwe kote hili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo ya maji.
Abdallah Rajabu , ameeleza kuwa wakati huduma nyingine za uboreshaji barabara zikiendelea greda zimekuwa zikikata mabomba ya maji na kisha wanatekeleza hivyo kusababisha wananchi kukosa maji.
Peter Nshimba,ameiomba serikali kutatua kero ya maji katika maeneo yao ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili