Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
SERIKALI imesema itahakikisha inaboresha ushirikiano na mataifa ya nje katika utendaji kazi kuhusu suala zima la ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kimtandao
Hayo yamesemwa jijini hapa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dk.Jim Yonazi wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wapelelezi pamoja na maaskari wa chumba cha mashtaka wa Tanzania na Zanzibar lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uhalifu wa Mtandao ambapo amesema Serikali itaendelea kufanyia kazi ya mashirikiano baina ya nchi yetu na nchi nyingine katika kuhakikisha tunaimarisha masuala ya mawasiliano ya TEAHAMA ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao.
Amesema Serikali itaendelea kuwalinda wananchi wake kutokana na uhalifu wa mitandao ili kuhakikisha nchi inakuwa salama.
“Uhalifu wa kimtandao ni Muhimu kutiliwa mkazo hasa katika zama hizi za kidigitali kwa kuwa uwepo wa usalama katika matumizi ya mitandano ni sawa sawa na kuhakikishia dunia inakuwa salama kwamfano kwasasa zaidi ya watu milioni 18 duniani ni watumiaji wa huduma ya mtandao (internet) idadi ambayo ni kubwa hivyo ni muhimu sana kuweka namna sahihi ya kulinda usalama wa watumiaji hao.,”amesema.
Aidha amesema kunahaja ya kujengeana uwezo kila mara kwa waliopata mafunzo hayo ili kwenda na ulimwengu wa kidigitali kutokana na uhalifu wa kimtandao ni mpana na kila siku teknolojia inakuwa.
Pamoja na hayo amesema Serikali imechukua hatua kwa kutunga Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ili kuweza kuweza kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa ukishika kasi.
Hata hivyo amesema walinzi hao wa usalama mtandaoni wanapaswa kushirikiana katika hatua changamoto zote uhalifu mtandao na kwamba Kwa kufanya hivyo watadhihirisha namna ambavyo Tanzania imejipanga katika kuhakikisha matumizi ya mitandao yanakuwa salama.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DCI),Camilius Wambura idara hiyo itahakikisha inaboresha mifumo ya kuhakiki uhalali wa taarifa zinazopitia kwenye mitandao ambayo imebuniwa na wataalam wa Teknolojia ya Habari nchini ili kuzuia matumizi mabaya ya mitandao.
“Makosa ya mtandao yanakuwa mengi na kusababisha uvunjifu wa amani na kuharibu furaha Kwa watu wengine,kupitia mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kutokana na mbinu mlizopata ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao kwani maarifa yatawasaidia katika kubadilishana taarifa,”amesema.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka wapelelezi hao pamoja na askari kuhakikisha wanazingatia misingi ya kazi na wito wa maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo.
“Mnapotoka hapa mkahakikishe mnafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi wenu kwani tabia za wachache zimekuwa zikiharibu taswira ya Jeshi jambo ambalo si jema,”amesisitiza.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais