Na Israel Mwaisaka,Timesmajira Online-Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere, amesema Serikali inakusudia kuboresha mpaka wa Kasesya unaounganisha nchi ya Tanzania na Zambia, ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Matai- Kasesya kwa kiwango cha lami.
Makongoro,ameyasema hayo baada ya kutembelea kituo cha forodha cha Kasesya wilayani Kalambo mkoani,ambapo amesema serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 inakusudia kuanza ujenzi wa majengo mapya ya taasisi za umma ikiwemo kituo cha polisi, uhamiaji , majengo ya ukusaji mapato (TRA) pamoja na nyumba za watumishi.
Pia aliwahakikishia wananchi wilayani humo, kukamilishwa kwa barabara ya Matai-Kasesya ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa bandari ya Kabwe,lengo likiwa ni kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda katika nchi jirani ikiwemo Kongo, Zambia na Burundi.
Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2024-2025 kituo cha forodha Kasesya wilayani Kalambo kilifanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato, kwa kukusanya kiasi cha billion 25.7 sawa na asilimia 172 kati ya lengo la kukusanya kiasi cha billion 14.

More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro