December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kuboresha huduma za afya Handeni

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Handeni


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali katika kipindi cha miaka miwili imeleta kiasi cha billion 6.7 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya uboreshaji wa huduma sekta ya afya.

Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Dkt. Mollel amesema kuwa amepokea maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ni ya kuangalia kwa karibu kwani iko karibu na barabara ya njia panda Chalinze kwenda Tanga ambapo kunatokea ajali nyingi hivyo lazima iwe na mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura yatakayo tokea wakati wowote.

Aidha ameeleza kuwa mpaka sasa katika hospitali hiyo huduma zinazopatikana ni pamoja na huduma za wagonjwa wa nje,X- ray,maabara na upasuaji.