January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali ifanye uhifadhi wa kisasa kuondoa migogoro ya ardhi

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini Aida Kenani (CHADEMA) ameishauri Serikali kufanya uhifadhi wa kisasa wenye manufaa na tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuondoa migogoro ya ardhi baina ya wanachi na hifadhi.

Aidha ameshauri kuboreshwa kwa kanuni za uhifadhi ambazo zimepitwa na wakati na hivyo kuwafanya wananchi kuendelea kuwa masikini kutokana na kulipwa fidia kidogo pindi mazao yao yanapoliwa na wanyama wanaotoka hifadhini huku wao wakitozwa faini za mamilioni ya shilingi pindi inapotokea amemjeruhi ama amemuua mnyama mkali wakati akitetea ili asimdhuru.

Kenani ameyasema hayo Feb 8,2024 wakati akichangia utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Ardhi, Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023.

Amesema ni vyema Serikali ikawa mfano kama inavyotaka wananchi wafuge kisasa kwenye eneo dogo,badi yenyewe iwe mfano hali itakayosaidia kupunguza ama kuondoa kabisa migogoro ya ardhi baina ya wananchi na hifadhi.

Aidha Mbunge huyo ameshauri Mamlaka za Serikali ziwasiliane pindi vijiji vinapoanzishwa ili kujua mapema kama eneo hilo ni sahihi kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli nyingine za kibinadamu ili kuondoa sintofahamu baina ya wananchi na hifadhi hapa nchini.

Kuhusu kanuni amesema kanuni za 2011   zinaleta doa kwenye Taifa na  sifa mbaya kutokana na kuthamini Wanyama kuliko binadamu.

“Kwa mfano katika eneo la kifuta machozi kwa binadamu  mwananchi akipata madhara kutokana na wanyama wakali na waharibifu,akijeruhiwa anatakiwa kulipwa kifuta machozi shilingi laki mbili,mkono au mguu ikikatika kabisa analipwa tena,akifa kifuta machozi ni sh.milioni 1,

“Yaan Taifa linaangalia thamani ya mwanadamu sawa na sh.mil 1?hili halikubaliki,tumeshafanya mabadiliko ya vitu vingi sana kuna shida gani kwenye kanuni hizi,

 “Kwenye mazao nako ni changamoto kubwa hawa wanyama wakali na waharibifu,huyu mwananchi ambaye amelima mita 500 kutoka eneo la hifadhi ,wanyama wakila heka  moja analipwa sh.25000 wakati mfuko mmoja wa mbolea unauzwa hadi sh 70000,sasa ekari moja ambayo angevuna zaidi ya gunia 25 ,na maandalizi yake mpaka anavuna ni takribani sh.750000 halafu Serikali inasema itamlipa 25000,

“Serikali ituambie ni wapi ataenda kununua gunia 25 kwa sh.25000,kanuni zinawapa umasikini watanzania,ukitoka kuanzia mita 501 mpaka kilomita moja anatakiwa alipwe sh.50000 kwa ekari hizi kanuni xifanyiwe marekebisho ili watanzania .”

Aidha amesema kutoka kilomita moja mpaka kilomita nne eneo la hifadhi  mwananchi kama wanyama wamekula mazao yake analipwa sh.75000 au 100000.

“Kanuni hizi waziri ana Mamlaka nazo  kwa nini tuanzungumza kila siku ,zinaleta sura mbaya nchini ,haipendezi,inawezekana kanuni zilikuwa zinafanya kipindi hicho kwa sasa zimepitwa na wakati maana huyo mwanadamu anapopambana na huyo mnyama mkali akimuua tu anatakiwa kulipa mil 30,kwa nini thamani ya mnyama iwe kubwa kuliko ya binadamu ni aibu kuendelea kujadili kanuni kama hizi ndani ya bunge hili ,”Tunategemea serikali inakwenda kulichukua hili jambo kwa umuhimu mkubwa najua hata TAWA kuna wakati wanasema sisi hatuwezi kuvuna hawa tembo ,badala yake wanawasukuma hifadhini

 Ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa mwananchi wake Shija Machenga kutoka kijiji cha Itete kata ya Itete  aliyekanyagwa na tembo mguuni Januari 27 mwaka huu.