Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Msanii Joyce Babatunde kutoka Senegal ndiyo amefungua siku ya leo ambayo ni ya tatu ya Tamasha la Wadau wa Muziki Afrika(ACCES) usiku huu katika viwanja vya Brake Point Dar es salaam kwa burudani kali yenye mahadhi ya Afro Fusion.
Mbali na msanii huyu wasanii wengine wanaotarajiwa kupanda jukwaani leo ni pamoja na mfalme wa singeli nchini, Sholo Mwamba, msanii wa Bongo fleva Maua Sama na kikundi cha Sanaa cha Sinaubi Zawose kutoka Dodoma.
Tamasha hili lilianza Novemba 24, 2022 na lina malizika leo kwa mafanikio makubwa likiwa limewajumuisha wadau mbalimbali wa sanaa na muziki kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wamebadilishana uzoefu.
Aidha, wanamuziki wa kitanzania wamejengewa uwezo na kufundishwa mambo ya tasnia hiyo ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa miziki Kwa njia za kisasa na uendeshaji wa tasnia hiyo kidijiti.
Tanzania ina kuwa nchi ya Tano Afrika kuwa mwenyeji wa Tamasha hili la Muziki Afrika tokea kuanzishwa kwake 2017.
Nchi nyingine zilizowahi kuwa mwenyeji ni pamoja na Senegal, Kenya, Ghana na Afrika Kusini.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA