Na. Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Sumbawanga
Serikali imewataka wananchi kutouza vifaa vya msaada walivyopatiwa kufuatia maafa ya upepo mkali uliosababisha nyumba 45 kuezuliwa na baadhi kubomoka katika kijiji cha Tamasenga kata ya Pito wilaya ya Sumbawanga mwaka jana.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga leo wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya kibinadamu vilivyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa kufuatia kuathirika na upepo mkali hapo Desemba 16, 2022.
Akizungumza kwenye hafla ugawaji wa vifaa hivyo, Sendiga alionya kuwa wananchi watakaobainika kuuza vifaa hivyo wajue wanaikosea serikali hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa kuwa vifaa hivyo lengo lake na kusaidia kaya zilizoathirika.
Sendiga alitaja vifaa vitakavyokabidhiwa kwa wahanga kuwa ni mahindi tani 9.2, ndoo 223, mikeka 200, magodoro 200, blanketi za wakubwa 200, sahani 256, vikombe 256 na sufuria 220.
More Stories
Rais Samia kupokea Tuzo ya ”The Gates Goalkeepers Award”
Walengwa wa TASAF watakiwa kujiandaa ukomo wa ruzuku
Kapinga:Azma ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote