March 15, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sema na Waziri kutatua changamoto za kisheria kwa wananchi

Na Mwandishi wetu

WIZARA ya Katiba na Sheria inatarajia kuzindua siku maalum itakayowapa wananchi fursa ya kuzungumza moja kwa moja na Waziri wa Wizara hiyo ili kuwasilisha na kupata ufumbuzi wa changamoto zao za kisheria.

Kwa mujibu wa taatifa ya Wizara ya Katiba na Sheria, hatua hiyo ni jitihada ya Serikali za kuwafikia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria na kuwapatia msaada kwa wakati.

Yaarifa hiyo imesema izinduzi wa siku hiyo maalum unatarajiwa kufanyika 17 Machi 2026, ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, atazindua rasmi utaratibu huo kupitia kituo cha huduma kwa mteja cha Wizara

Imeelezwa kuwa kupitia utaratibu huo wananchi watapata fursa ya kupiga simu katika kituo hicho kupitia namba 0262160360 au 0800004004, ambapo simu zao zitapokelewa moja kwa moja na Waziri wa Katiba na Sheria ili kusikiliza changamoto zao na kuzitolea ufumbuzi.

Mpango huo unalenga kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma na ushauri wa kisheria kwa wananchi.