January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekta ya utangazaji yahimizwa kuzingatia sheria, kanuni

Grace Gurisha, TimesMajira Online

SERIKALI imehimiza watoa huduma za mawasiliano nchini kuzingatia Sheria na Kanuni ziliwekwa kwenye leseni katika utoaji wa huduma husika kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawaailiano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari wakati akizindua kikao cha Watoa Huduma za Utangazaji na Maudhui, Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilishirikisha wadau mbalimbali kutoka kwenye makampuni ya habari wakiwemo Azam Media, Multchoice Tanzania limited, Watoa Huduma kwa njia ya Cable, COSOTA na Shirikisho la  Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Dkt. Bakari, amesema baadhi kanuni za maidhui na utangazaji zinafanyiwa maboresho na zinatarajia kuanza hivi karibuni, ambapo TCRA imeboresha utendaji kazi zake kwa kuweka mifumo madhubuti zaidi na imeendelea kutoa ushauri kwa watoa huduma kila mara.

Amesema, kikao hicho shirikishi pia kilihudhuliwa na watoa huduma za utangazaji na maudhui kutoka vyombo vya habari mbalimbali. 

Mkurugenzi huyo, amesema lengo la  kikao hicho kilichoratibiwa na TCRA Kanda ya Kati, kililenga kutoa elimu ya namna bora zaidi katika kufikisha maudhui kwa walaji bila kuwa na migongano baina ya watoa huduma.

Pia kikao hicho kimependekeza wanaochakata maudhui kuangalia namna nzuri zaidi ya kuzuia maudhui yasiyo na staha kwa jamii ili kuondoa malalamiko ndani ya Jamii.  

Kikao hicho kimependekeza pia vikao kama hivyo viwe vinafanywa mara kwa mara ili kuongeza ufahamu zaidi kwa watoa huduma na Mamlaka za Serikali zinazosimamia sekta ya maudhui ya Utangazaji.Â