Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DODOMA
Wizara ya Madini imedhamiria kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa katika Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko Juni 23, 2023 alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Shirikisho Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa na wachimbaji hao jijini Dodoma.
“Shabaha ya Wizara ya Madini Mwaka wa Fedha 2023/24 ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuwainua wachimbaji wadogo waweze kukua na kufanya vizuri katika uchimbaji,” amesema Dkt. Biteko.
Aidha, amewataka wachimbaji wadogo nchini kushirikiana katika shughuli za uchimbaji wa madini ili kukuza uchumi wao na kuongeza mchango wao katika Pato la Taifa.
Kikao hicho kifupi kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Katibu Mtendaji Tume ya Madini Eng. Yahya Samamba, Kamishna wa Madini Dkt. Abdul Rahman Mwanga na Watendaji wengine wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa