March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekretarieti ya CCM yatathmini mwenendo uchukuaji fomu

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

SEKRETARIETI ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, imekutana kwa ajili ya kufuatilia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu kwa ngazi ya Ubunge na Udiwani.

Kikao hicho kilichokaa Juni 28,2025,kilipokea na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo lililoanza rasmi siku hiyo kwa mchakato wa ndani ya CCM nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania kuteuliwa ndani ya CCM,limeanza Juni 28, 2025, saa 2:00 asubuhi na litahitimishwa Julai 2, 2025, saa 10:00 jioni.

Pia ratiba hiyo itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za Ubunge wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum, Udiwani wa Kata au Wadi na Udiwani wa Viti Maalum.